Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo akiweka bayana lengo la wawo kuweka kambi jimboni hapo. |
Jeshi la Polisi nalo halikuwa mbali kuimalisha ulinzi na usalama katika eneo hilo la tukio |
Baadhi ya waumini na wachungaji wa kanisa hilo wakiendelea na mapambio nje ya kanisa hilo kama walivyo kutwa na mpiga picha wetu. |
Makamu Mwenyekiti wa kanisa hilo Ndugu Zakalia Schone akizungumzia sakata hilo. |
wafanyakazi wakiwa hawaamini kinachotokea jimboni hapo |
jeshi la polisi wakiwa katika doria nje ya kanisa hilo |
Baadhi ya wachungaji wa shirika mbalimbali mkoani mbeya katika kanisa la Moravin wakiwa nje ya kanisa hio kusubiri hatma ya mgogoro wao na Askofu Mkuu wa jimbo hilo kujiudhuru kwa madai mbalimbali. |
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya Ndugu Richard Mchomvu akizungumza na waumini hao kwa lengo kusitisha maamuzi yao ya kuendelea kuzifunga ofisi hizo za jimbo. |
Wachungaji na waumini wa kanisa hilo wakifanya maombi ya pamoja mara baada ya kumaliza kumsikiliza Mkuu wa Wilaya Dakta Nouman Sigala nje ya uzio wa kuingilia Kanisani hapo. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la
Kusini Magharibii, leo wamezifunga ofisi za Jimbo hilo zilizopo eneo la jacaranda
jijini Mbeya , wakishinikiza kujiudhulu kwa Askofu wa Jimbo hilo
Alinikisa Cheyo kujiudhuru wadhifa wake.
Madai mengine
ya waumini na wachungaji hao ni pamoja kushinikiza kuitishwa kwa
halmashauri ili waitishe Sinodi ambayo ndiyo yenye maamuzi ya mwisho
kuhusiana na mgogoro huo.
Hatua hiyo ya kuzifunga
ofisi hizo, imekuja ni baada ya kuwepo kwa mgogoro uliodumu kwa
mwaka mmoja na nusu ukihusisha ofisi ya halmashauri Kuu ya Jimbo la
Kusini Magharibi dhidi ya Mchungaji na Mwenyekiti wa Jimbo hilo Nosigwe Buya
na Askofu Alinikisa Cheyo.
Waumini wa Kanisa hilo
pamoja na wachungaji, wamekuwa wakimtuhumu Askofu wa jimbo hilo ya kwamba
amekuwa akikiuka Katiba ya Kanisa kwa kuingilia baadhi ya shughuli ambazo
hazimuhusu.
Moja ya mambo
yanayotajwa kuingiliwa na Askofu huyo yakiwa ni kinyume cha taratibu na sheria
zilizomo kwenye Katiba yao ni kufanya maamuzi ya kumsimamisha kazi aliyekuwa
Mwenyekiti wa jimbo hilo Mchungaji Buya kinyume cha taratibu.
Wakizungumza katika eneo
la tukio baadhi
ya waumini na wachungaji ambao walikuwa kwenye eneo la tukio, wamesema
Askofu Cheyo amekuwa akisahau wajibu na majukumu yake ya kiroho na
ushauri na kuingilia masuala ya kiutendaji zaidi.
Wamesema, hali
hiyo inatokana na dhamira mbaya aliyokuwa nayo askofu huyo ya
kutaka kufanya jaribio la kumuondoa Mwenyekiti Mchungaji Nosigwe Buya huku
akijua kabisa anafanya makosa kikatiba kwa kufanya mapinduzi.
Akisimulia chanzo cha
sakata hilo kutokea Mchungaji Chile amesema, mgogoro huo
ulianza 30/4/2014 ambapo halmashauri kuu ilikutana na kujadili agenda juu
ya utendaji mbovu wa kamati tendaji na katika kikao hicho walimtaka
Mwenyekiti kutoa tahalifa ya shilingi milioni 200 ambazo zilikuwa za
ujenzi wa Sekondari ya Mbozi.
Pia, Makamu wa kanisa
hilo Zakaria Sichone kutakiwa kuwasilisha taarifa ya maandishi ya
jinsi alivyotimiza wajibu wake kikatiba ya kusimamia ujenzi wa majengo hayo ya
shule lakini taarifa hiyo ilikataliwa kutokana na kuwepo kwa kasoro nyingi.
Amesema, wakiwa ndani ya
kikao hicho, Askofu Cheyo aliamuru Mwenyekiti Buya na Makamu wake
watoke nje ya kikao jambo ambao ni kinyume cha Katiba kwani yeye nafasi yake ni
kushauri na si kufanya maamuzi kama mjumbe.
Amesema, Askofu huyo
tena akiwa anafahamu Katiba ya Kanisa inasema nini, alishindwa kutoa ushauri
kwa wajumbe walioshiriki kikao cha kuwajadili Mwenyekiti Buya na makamu wake
ambacho kilitoa maamuzi ya kuwatoa nje kisha kufanya uchaguzi mpya na
kumchagua Mwenyekiti Hakimu Mwandanuka kukalia kiti
hicho.
Aidha, waumini hao ambao
walizifunga ofisi hizo kwa zaidi ya masaa matano waliweza kuzifungua baada ya
kuwasili kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nomarn Sigalla ambaye
aliwaomba kutulia kwani serikali inalifahamu tatizo hilo na kwamba imepanga
kukutana na uongozi wa pande zote mbili(kesho) leo..
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269