NA MWANDISHI MAALUM, MTWARA
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amempa
muda wa miezi miwili mkandarasi anayejenga barabara ya Ndundu-Somanga kufanya
kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo haraka bila kutoa visingizio
vyovyote.
Waziri wa Ujenzi aliitoa kauli hiyo leo katika
kijiji cha Manzese, Wilayani Kilwa
mkoani Lindi wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo la ujenzi.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa mkandarasi huyo
ameshalipwa fedha zote alizokuwa ana dai hivyo anachotakiwa ni kufanya kazi
kila siku usiku na mchana ili amalize kazi hiyo haraka,
“Tunataka mpaka mwezi wa tisa, tuone barabara ya
lami na sio vinginevyo, wahandisi wote wa mkoa wa Pwani na Lindi wamsimamie
kwelikweli na kwa muda wote ili aweze kukamilisha kazi hii kwa muda tuliompa”
Alisema Waziri Magufuli.
Pia waziri wa Ujenzi aliwaasa Wananchi kutomwibia
Mkandarasi huyo Mafuta ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
“Msiibe mafuta kwa mkandarasi pia nayeye anatakiwa
awalipe vizuri wafanyakazi wake kwasababu sisi pia tunamlipa vizuri, pia anatakiwa
atunze vifaa vyake vizuri” alisema Waziri Magufuli.
Kuhusu barabara ya kutoka Lindi kuelekea Mtwara
katika baadhi ya maeneo, Waziri Magufuli amewataka viongozi wa mkoa kusimamia
malori yanayobeba gipsam na mawe makubwa kupita kiasi hali inayohatarisha
usalama wa barabara hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269