Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akifafanua jambo kwa Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO. Bw. Al Amin aliambatana na wadau wa maendeleo Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga (hayupo pichani). Kulia ni Afisa Miradi kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko. wengine wakinamama wakikundi cha kimasaia waliofika kupokea ugeni huo.
Na Mwandishi wetu
Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni duniani (UNESCO) limezitaka redio za
jamii kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii hususan
ukeketaji kwa akina mama kwa kuelezea athari zitokanazo na ukeketaji
ili kuisaidia jamii yenye mila hizo kuachana nazo kabisa.
Hayo
yamebainishwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph wakati wa ziara ya kutembelea miradi kwenye
vijiji vya Ololosokwani wilayani Ngorongoro na kuzitaka redio za kijamii
kuwa sehemu ya kutoka elimu ya katiba ili kuiwezesha jamii kufahamu
wajibu wao kama raia ili wakati unapofika waweze kufanya maamuzi sahihi
ya maendeleo.
Al
Amin alisema kuwa vipindi vya elimu ya Afya na masuala ya kijamii
yahusuyo serikali na jamii kwa ujumla yanapaswa kupewa kipaumbele na
redio hizi katika masuala ya huduma za kijamii hususan ndoa za utotoni,
ukeketaji na ajira za utotoni ili ziweze kukomeshwa katika jamii kwani
zinarudisha maendeleo ya mtoto hasa wa kike.
“Kwa
sasa hapa nchini kumekuwa na mjadala wa Katiba Mpya mchakato
unaoendeshwa na Bunge la Katiba linaloendelea na vikao vyake mjini
Dodoma. Wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea, kushiriki
katika mijadala mbalimbali itakayosaidia kupanua uelewa wao ili mwisho
wa siku wanajamii waweze kuwa na maamuzi sahihi na hilo ndio lengo la
redio” alisema Al Amin.
Alisema
kuwa japo matangazo yamekuwa ya muda mfupi redio Loliondo imekuwa
faraja na imetoa mchango mkubwa katika kusaidia jamii kupata uelewa
kwenye masuala mbali mbali ya kijamii hususan wizi wa mifugo na utunzaji
wa mazingira ya kiikolojia kwenye maeneo husika kwenye uwanda wa eneo
la pori tengefu la Loliondo.
Nae
Mkurugenzi wa RAMAT Yannick Ikayo ambayo inaendesha mradi wa redio ya
kijamii ya Loliondo FM alisema kuwa redio hiyo imekuwa mkombozi kwa
kutoa elimu kwa jamii na imesaidia kuongeza uelewa na madhara mbali
mbali kwenye masuala ya kijamii hususan ukeketaji na utunzaji wa
mazingira ya kijamii.
“Migogoro
ya kijamii imekuwa ikipatiwa ufumbuzi hali inayoifanya jamii ya
kifugaji kufaidika na redio hii kwani imekuwa na msaada mkubwa kwa jamii
yetu na wilaya kwa ujumla hivyo tunaiomba jamii kuipa ushirikiano na
kuamini kuwa redio hiyo ni mkombozi wao na kiunganishi kati yao na
watawala”, amehitimisha Ikayo.
Wilaya
ya Ngorongoro imeonekana kuwa na changamoto katika elimu hasa vijana wa
kike kuacha masomo kwa ajili ya kuolewa na wengine kukimbia kukeketwa
hali inayohitaji serikali kutoa elimu kubwa kwa jamii ya kifugaji
kuachana na mila potofu ikiwemo ukeketaji ulioshamiri.
Wanahabari
walitembelea wilayani humo waliwashudiwa wasichana kutoka kabila la
kifugaji wakiwa tayari wamekeketwa kwa kuvalishwa mavazi maalum
yanaonyesha kutoka kwenye tohara huku wakimshuhudia msichana
aliyeshindwa kwenda kujiunga na kidato cha kwanza akiuza mkaa kwa
kisingizio cha kukosa ada.
Sehemu maalum ya anayotumia mtoa huduma wa maktaba hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo kutokana na shida ya umeme katika eneo hilo Kompyuta hiyo inatumia umeme wa jua (solar).
Jengo la Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO iliyopo kwenye kijiji cha Ololosokwani wilayani Ngorongoro kwa uangalizi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT. Loliondo FM Redio ilianzishwa mwaka Oktoba 2013 pamoja na Maktaba na Ujenzi wa Kituo cha Utamaduni ambavyo lengo ni kusogeza elimu kwa jamii ya kifugaji na kupata uelewa wa masuala mbali mbali yanayowazunguka ikiwemo utunzaji wa mazingira.
Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo (wa pili kushoto) akielezea maendeleo ya miradi mbalimbali inayosimamiwa na Shirika lake ikiwa chini ya ufadhili wa UNESCO kwa ugeni ulioambatana na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (katikati) wakati wa ziara ya kukagua miradi hiyo.
Baadhi watoto wa jamii za kifugaji wa kijiji cha Ololosokwani ambao wanastahili kupata elimu ya awali lakini wazazi huwaamuru kwenda kuchunga mifugo kama walivyokutwa na mpiga picha wetu kwenye maeneo ya kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269