Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwakaribisha wadau wa maendeleo ofisini kwake Loliondo walioongozwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa tatu kushoto) aliyefuatana na Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania , Bw. Slyvester Nteere (wa pili kushoto) pamoja na mwakilishi wa Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Eric Kalunga (kushoto) wakiwa na mwenyeji wao Diwani wa kata ya Ololosokwani, Yannick Ndoinyo (kushoto kwa DC).
Na Mwandishi wetu, Ngorongoro
Serikali na halmashauri wilayani Ngorongoro zimetakiwa kutoa ushirikiano kwa redio za kijamii wilayani humo kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi wao.
Hayo yameelezwa na Meneja wa redio ya kijamii ya Loliondo FM, Joseph Munga, wakati wa ziara ya kukagua miradi inayoendeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) redio hiyo ikiwa miongoni mwa miradi inayofadhiliwa na UNESCO wilayani hapa wakiambatana na wadau wa maendeleo kutoka kampuni ya Samsung na Ubalozi wa Uswiss hapa nchini.
‘Redio za Jamii ndio chombo pekee kinachoziunganisha serikali na jamii katika suala zima la kujiletea maendeleo’ alisema Joseph Munga.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali akiwa kwenye mazungumzo na wadau wa maendeleo waliofika wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kushoto) ambaye pia ndio mkuu wa msafara huo akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali wakati wa mazungumzo hayo. Kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni a Samsung tawi la Tanzania, Bw. Slyvester Nteere.
Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo juu mradi waliobuni wa kituo cha utamaduni wa Kimasai ambao uko mbioni kuanza ujenzi wake wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika hilo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili lulia) akitoa ushauri kuhusu kituo hicho kuwa kitakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa jamii hiyo ya kifugaji pindi kitapokamilika huku akisisitiza kuwa mipango iliyopangwa kama walivyopewa maelezo iendane na wakati.
Mmoja wa wadau wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini, Bw. Erick Kalunga akisoma moja ya vitabu ndani ya maktaba hiyo inayofadhiliwa na UNESCO, Maktaba hiyo inayotumiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Ololosokwani na vijana wa kata hiyo.
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (kulia) ambaye pia ni mkuu wa msafara huo wa kukagua miradi inayofadhiliwa na UNESCO akiteta jambo na Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere ndani ya maktaba hiyo. Anayefuatilia mazungumzo hayo kwa karibu ni Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (katikati).
Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) akitoa maelezo baada ya kutembelea Maktaba inayofadhiliwa na UNESCO nje ya maktaba hiyo.
Kikundi cha ngoma ya Kimasai kilichowatumbuiza wageni waliotembelea mradi wa redio ya Loliondo FM inayofadhiliwa na UNESCO wakitumbuiza wakati wa ziara hiyo.
Afisa Miradi wa kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO, Myoung Su Ko, akijumuika na kinamama wa kikundi cha ngoma za kimasai kutoka kata ya Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Diwani wa kata ya Ololosokwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisiolo la kiserikali la RAMAT inayomiliki Redio Loliondo FM, Bw. Yannick Ndoinyo akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ikiwemo maktaba, redio na ugawaji wa vitabu vya masomo ya Sayansi na hesabu vinavyoafadhiliwa na UNESCO kwenye kata hiyo.
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akitoa pongezi kwa redio Loliondo FM kwa kuweza kuihamasisha jamii inayoizunguka kwa kuburudisha, kutoa elimu na habari kwa ujumla hiyo sio kazi nyepesi kutokana na uchanga wenu wa redio yenu.
Meneja Mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere akikabidhi zawadi kwa kikundi cha ngoma cha kinamama wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi inayofadhiliwa na UNESCO kwenye kata ya Ololosokwani.
Wanakikundi cha ngoma na wakazi wa kata ya Ololosokwani wakiangalia taarifa mbalimbali za mitandao kwenye “Tablet” inayotengenezwa na kampuni ya Samsung wakati wa ziara hiyo.
Mmoja wa wanakikundi akitumia Tablet kupiga picha wanakikundi wenzake pamoja na wadau wa maendeleo (hawapo pichani).
Wanakikundi cha ngoma za kimasai wakiwa kwenye picha ya pamoja na ugeni huo huku wakionyesha furaha baada ya kupokea zawadi ya fulana kutoka kampuni ya Samsung.
Meneja wa redio jamii ya Loliondo FM, Joseph Munga akiwa kwenye studio za redio hiyo wakati wa ziara ya UNESCO kukagua miradi inayoifadhili.
Meneja mauzo wa Samsung tawi la Tanzania, Bw. Sylvester Nteere (aliyeketi) akiwa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph ndani ya studio za kurushia matangazo za redio ya Loliondo FM inayorusha matangazo yake kwenye mnara wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na kuifika jamii kubwa kwenye maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269