Breaking News

Your Ad Spot

Aug 2, 2014

WAZIRI AMOS MAKALLA AFIWA NA BABAKE MZAZI


                                                         Marehemu Gabriel Makalla



Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla anasikitika kutangaza kifo cha babake mzazi, Gabriel Makalla kilichotokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.


Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa waziri Palm Residence Ocean Road namba 18E Dar es Salaam, Mwili utaagwa Jumapili katika Kanisa la Azania Front saa 6 mchana.


Baada ya hapo mwili utasafirishwa kwenda Mvomero kwa mazishi yatakayofanyika Jumatatu saa 7 mchana. 



Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi,  amina.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages