Breaking News

Your Ad Spot

Aug 7, 2014

ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI MAREKANI

KIKWETE: TUNAKWAMISHWA NA UZALISHAJI NA MATUMIZI MADOGO MNO YA UMEME

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014.

 NA MWANDISHI MAALUM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi yachini mno ya umeme.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko lauzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrikana kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakatialipozungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara laAfrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye nimwenyeji wa Mkutano huo.

Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi waMikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bilaongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika halitatokakwenye uduni.

Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la Umojawa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan AfricanCountries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni asilimia 31 tu nahivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani.

Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umemeya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi wa Barahilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila
raia wa Marekanianatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati 440.Ameongeza Rais Kikwete:“Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya umemekwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”

Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tuya Ulaya – Hispania.
Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa Afrika zinauwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho kinazalishwa na nchi mojatu ya Marekani Kusini ya Argentina.”

Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi zisizokuwa zakiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu, ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu nauboreshaji wa kilimo.

Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidiakuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya teknolojiaya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza demokrasia, utawala borana utawala wa sheria.

Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi waTanzania.

 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti 6, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014

Viongozi wa Afrika wakisalimiana kwa furaha baada ya kupata picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakipata picha ya kumbukumbu na mwenyeji wao Rais Barak Obama wa Marekani wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014


RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI




 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  aliyemtembelea kumjulia hali kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina  ya nchi hizo mbili.
 Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Mama Salma Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe   kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao  walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
 Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  akiomngea na  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe   kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani,  alipomtembela kumjulia hali Rais Kikwete. Viongozi hao  walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika,  wakiongea kwa furaha walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya  nchi hizo mbili.
Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa furaha na mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages