Breaking News

Your Ad Spot

Sep 6, 2014

DAMU YA WALIOPONA EBOLA KUTUMIKA KUUGUZA WAGONJWA WENGINE

Mkutano wa WHO kuhusu Ebola mjini Geneva.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine.
 
Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.
 
Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
 
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili. Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana. Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages