Breaking News

Your Ad Spot

Sep 7, 2014

DIAMOND AMTIA MATATANI PROMOTA WA KI-NIGERI, UJERUMANI

FUJO ZA 30.8.2014 KATIKA SHOW YA DIAMOND HASARA EURO 300,000

PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI

POLISI WASEMA MPAKA KIELEWEKE, M-NIGERIA ROHO JUU

Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya african paty na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe,kwa promota huyo.
Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.
 
Taarifa za uhakika polisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt) ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS, Polisi inaendelea kumuhoji kwa kujihusika na biashara zingine haramu.

Wakati huo huo tahasisi mbali mbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemie za kuwadanganya washabiki na kulivunjia adhi sifa za bara la Afrika nchini ujerumani ,tahasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na m-nigeria huyo Britts Events au Awin Williams Akpomiemie,Pia magazeti mbali mbali ya ujarumani na nchi za kiafrika yameandika BRITTS MAFIA HITS STUTTGART,GERMANY AGAIN !! mojawapo ya gazeti la ghana soma; http://www.modernghana.com/news/567209/1/african-diaspora-is-still-bleeding-diamonds-nightm.html
 Mashabiki wakiwa wamechanganyikiwa baada ya kugundua kuwa 'wameingizwa mjini' kwa onyesho la Diamond kutofanyika
 Hali ya ukumbi ilivyosalia baada ya timbwili la mashabiki baada ya kukosekana onyesho la Diamond
 Polisi wakifanya kazi ya ziada kutawanya mashabiki ili kuokoa Diamond
 Dianond akitoroshwa kwa gari baada ya polisi kumuokoa asiingie mikoni mwamashabiki
 Mashabiki wakilizonga gari alimokuwa Diamond

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages