Breaking News

Your Ad Spot

Sep 9, 2014

WANACHAMA WA VICOBA KATA YA KIWERE WAMPONGEZA MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA KWA KUWAONGEZEA NGUVU

Mbunge  wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa kushoto akipongezwa na mmoja kati ya  wapiga kura wa kijiji cha Kiwere
Mfanyabiashara  wa  nyama  choma Kiwere  kulia akimweleza  mbunge  Mgimwa  jambo baada ya kutembelea  vijana  na  wananchi  wanaojishughulisha na biashara eneo la magenge ya Kiwere 
wanakikundi  cha uoteshaji  miti Kiwere wakimweleza  mikakati yao mbunge Mgimwa katikati 
Mbunge wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa akipita kwa shida katika  vichaka baada ya kwenda  kuwatembelea  wapiga kura  wake  kijiji  cha Kiwere 
Kama  anazungumza   vile "lazima nimefike  kuona kazi za  wapiga kura  wangu "

DIWANI VITI MAALUM CCM LUDEWA AFARIKI DUNIA

diwani  wa  viti maalum  Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta) . wa  tatu  kulia  akiwa na mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kulia na katibu wake Stan Gowele  na wananchi9  wengine wa Ludewa  wakijiandaa kunyanyua nguzo ya  umeme  enzi wa uhaki wake  wiki mbili zilizopita 
 Wananchi  wa Lupingu  Ludewa  wakilitazama  daladala  lililopata  ajali  na kusababisha  kifo cha aliyekuwa  diwani wa viti maalum kata ya  Lupingu Prisca  Kayombo  leo
Diwani wa  viti maalum  Lupingu Prisca Kayombo (Zaruta) akishiriki kubeba  nguzo ya  umeme
Diwani wa viti maalum Lupingu Prisca Kayombo(Zaruta)  kulia  akishirikiana na mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  kufukia  nguzo za umeme  kwenda kata ya Lupingu katika kijiji cha Ntumbati wiki  mbili kabla ya  kifo chake leo 
Gari ya wagonjwa ikiwashusha majeruhi katika Hospitari ya wilaya ya Ludewa waliokuwamo katika ajari hiyo
 majeruhi wakishushwa hospitari
 Wananchi wa kata ya Ludewa wakishuhudia majeruhi waliokuwa wakishushwa katika gari ili kuwatambua
                               Habari na  picha na   Matukiodaima.co.tz

DIWANi  wa  viti maalum kata ya Lupingu  wilaya ya  Ludewa Prisca Kayombo(Zaruta) amekufa  papo hapo na wengine kujeruhiwa  vibaya katika ajali ya  ajali mbaya ya gari  iliyotokea  leo asubuhi.

Mashuhuda wa  ajali  hiyo  waliozungumza na mtandao  huu  walidai kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni gari hilo ambalo  walikuwa  wakisafiriki  kutoka  Lupingu - Ludewa  kufeli  breki na hivyo  kupinduka .

Credo Haule  alisema kuwa  baada ya  gari hilo aina ya Toyota Costa inayojulikana kwa jina la DMX iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Ludewa Mjini kuelekea Lupingu ,kufeli  breki dereva  aliwataka  abiria  kutulia ndani ya  gari  hilo ila  diwani huyo hakuweza kufanya  hivyo na kuamua  kuchukua maamuzi magumu ya kutaka  kuruka katika gari  hilo.

Alisema  kuwa  wakati akiruka  alimsukuma  utingo wa  basi hilo na hivyo  wote  wawili utingo na diwani  kufunikwa na gari hilo na kupelekea kifo cha  diwani  huyo  huku utingo  huyo akiwa mahututi  baada ya  kubanwa na gari hilo.

" Diwani  huyo amepoteza maisha  wakati akiwa njiani kuelekea  kujumuika na  wananchi wake katika  shughuli ya  maendeleo ya  kuchimba mashimo ya nguzo za umeme  kuelekea kijijini kwake  Lupingu"

Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe ameeleza  kusikitishwa na kifo  cha  diwani  huyo  kutokana na mchango  wake mkubwa aliouonyesha  enzi wa uhai  wakati kwa kushiriki  vema na  wananchi wa kata  yake katika zoezi la kufyeka na kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu.

Alisema  kuwa anakumbuka  ni wiki  mbili  pekee  zimepita  toka diwani  huyo  alipoungana nae katika  uchimbaji wa mashimo ya nguzo za umeme  kwenda kijiji cha Ntumbati na kuwa  hata wakati ajali  hiyo inamkuta  bado  alikuwa katika harakati za kuwatumikia  wananchi  wake.

" Ludewa  tumempoteza  diwani mchapa kazi na aliyependa  kujituma muda  wote na hata  wakati  mwingine diwani  huyo alikuwa akifanya kazi  ngumu kama mwanaume  kwa  kubeba  nguzo za umeme kwa  kushirikiana na mimi na wananchi  wake .....kwweli kifo  chake ni pigo kubwa  ndani ya CCM na kwa  wananchi  wa kata  nzima ya  Lupingu"

Kwani kati ya madiwani  waliokuwa  bega kwa bega na wananchi  wao na mbunge ni pamoja na diwani  huyo ambae  alikuwa mstari wa mbele  kuona kata ya Lupingu inapata  umeme wa uhakika baada ya  miaka zaidi ya 50 ya Uhuru  bila umeme .

Mbunge  Filikunjombe  alisema  atamkumbuka  diwani  huyo kutokana na mchango  wake mkubwa katika maendeleo na vile  alivyofanya kazi na wananchi wote  bila  kujali itikadi zao za vyama.

Mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa Juma Madaha  amethibitisha  kutokea kwa  ajali  hiyo  iliyosababisha  kifo cha  diwani  huyo na kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2  asubuhi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages