Breaking News

Your Ad Spot

Oct 19, 2014

IPTL YAJA NA WANASHERIA KUTOKA MAREKANI KUHUSU MGOGORO UNAOIKUMBA

Wanasheria kutoka Ulaya na Marekani wanaoiwakilisha Kampuni ya Uwekezaji ya VIP Engineering and Marketing Limited wameibua wanachodai ni ukweli juu ya mgogoro unaoikumba Kampuni ya Kufua Umeme hapa nchini ya IPTL. 

Katika kueleza ukweli huo, Wanasheria hao waliongozwa na maswali yafuatayo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari yaliyofanyika jijini Arusha leo. 

 Miongoni mwa maswali waliyoulizwa Wanasheria hao yalikuwa yanahusu mada zifuatazo: 

 1. Kueleza historia fupi ya mgogoro wa IPTL tangu ulivyoanza hadi sasa. 

 2. Kueleza msimamo wa VIP Engineering and Marketing Ltd kuhusu Akaunti Maalumu (Escrow Account) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). 

 3. Kueleza kwa nini Akaunti Maalumu (Escrow Account) ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. 

 4. Kama hisa za IPTL zingetolewa kwa mtu mwingine zaidi ya PAP, kwa mfano, Benki ya Standard Chartered; Je ni kweli kuwa mnunuzi yeyote wa hisa za IPTL angeweza kuwa na haki juu ya Escrow Account? 

 5. Baadhi ya wahisani wametangaza kusitisha kuunga mkono bajeti ya Serikali kwa kuwa wanaamini kwamba kuna ufisadi kwenye fedha zilizokuwa kwenye Escrow Account. Upi ni ushauri wao kwa serikali ya Tanzania juu ya suala hilo. 

 6. Je Benki ya Standard Chartered inayo madai yoyote dhidi ya IPTL na kwenye akaunti maalumu (Escrow Account). 

 7. Kama wanauamini mfumo wa mahakama za Tanzania 

 8. Nini msimamo wako kuhusu madai yanayotolewa eti kwamba Mahakama za Tanzania zinanuka rushwa. 

 9. Baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini zimetangaza kuwa Benki ya Standard Chartered imefanikiwa kupata amri ya mahakama huko Uholanzi kukamata mali za VIP Engineering and Marketing Ltd zilizoko katika nchi hiyo. Je kuna ukweli juu ya taarifa hizo. Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

 TUTAWALETEA MAJIBU YA MASWALI HAYO KWA KIREFU NA KWA UFASAHA BAADAYE.
Wakili kutoka Uholanzi Dk.Camilo Schutte akifafanua 
jibu lake kwa waandishi wa habari jijini Arusha leo.
Wakili kutoka Marekani Chris Provenzano naye akitoa
 ufafanuzi baada ya kuulizwa swali.
Mwanahabari Faustine Kapama akiongoza mahojiano hayo.
Wanasheria wa kampuni hiyo wakipitia baadhi ya taarifa kwenye mtandao wakati wakijibu maswali ya wanahabari. Kushoto ni Wakili wa Kitanzania wa Kampuni ya VIP, Resipius Didace.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya VIP, 
James Rugemalira (kulia), akiwaelekeza jambo mawakili hao. 
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya VIP, 
James Rugemalira (kulia) akiangalia moja ya taarifa zinazohusu Kampuni ya IPTL akiwa na  wakili wake kutoka Uholanzi. 
Wakili Camilo kutoka Uholanzi, akifafanua jambo mbele ya wanahabari. Kulia ni Wakili Didace.
Mawakili hao kutoka ulaya wakiteta jambo wakati wakitoa 
majibu kwa wanahabari.
Mwanahabari Jamila Omary akichukua taarifa hiyo.
Mpiga picha Dotto Aristrides wa Kituo cha Channel Ten akichukua kumbukumbu za mahojiano hayo. Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages