Breaking News

Your Ad Spot

Nov 1, 2014

JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE

 *VIONGOZI WATAKIWA KUWA WABUNIFU JUMUIAN IKUE KIUCHUMI

Dar es salaam, Tanzania

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seif Shaban Mohamed, amewataka viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.

Mohammed ametoa agizo hilo leo, wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Arnatouglou, mkoani humo.

"Nawapongezeni kwa kuunda kamati ndogondogo ndani ya jumuia, kufanya hivi kuutasaidia kusogeza huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo kukifanya chama chetu kiendelee kuaminiwa" alisema Mohamed.

Alisema Jumuia inazo rasimali nyingi hivyo ni vizuri sasa zikatumika ipasavyo kukuza uchumi wa jumuia ya Wazazi na viongozi wa jumuia wasipende kusubiri kila kitu muelekezwe na viiongozi wa juu.

Alitoa mfano wa kitegauchumi cha Jumuia hiyo kilichotelekezwa bila kuendelezwa kuwa nieneo la shule ya jumuia hiyo ya Boza iliyopo mkoani Tanga, ambapo alisema  kuwa ina ardhi ya kutosha lakini haifanyiwi uzalishaji mali wowote.

Mohamed alipongeza Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha daftari hilo la wanachama akisema litasaidia kuwatambua wanachama wao kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa hivyo kurahisisha shughuli za kisiasa kwa kutambuana katika chaguzi mbalimbali na shughuli nyingine kama za maendeleo.

Katika hatua nyingine Mohamed alisema wanajumuia wote ya wazazi wanaiunga mkono Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalumu la Katiba na kuwa wao wanautaka muundo wa serikali mbili kwani ndio utalipeleka mbele Taifa la Tanzania.
 
Alitoa mwito kwa wanachama wote wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuwachagua viongozi wao kuanzia ngazi za mashina wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika hivi karibuni.

Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Ali, alisema mpango wa kuanzisha daftari hilo ni moja ya mikakati yao ya kuibadilisha jumuia kiutendaji.
 
"Hii jumuia yetu kwa muda mrefu ilikuwa nyuma kimaendeleo lakini tumedhamiria kuibadilisha na kuwa ya kiutendaji zaidi na ndio maanna tumeanzisha kamati ndogo ndogo za maendeleo na kuwateua watu wenye sifa za kuziongoza yaani wenye taaluma" alisema Cholaje

Aliwataka viongozi wote waliochaguliwa kujitambua kuwa wamechaguliwa si kwa bahati mbaya bali ni kwa ajili ya kuonekana kuwa wana uwezo wa kuleta maendeleo ndani ya jumuia hiyo.

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seif Shaban Mohamed (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Daftari la wanachama wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Arnautoglo. Kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Ali.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje wakionyesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa.

 Viongozi wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje ,  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed, Katibu wa Elimu na Malezi Taifa, Masoud Bwire na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Dar es Salaam, Nicolaus Msemo.
 Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje, akizungumza katika uzinduzi huo.
  Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje (kushoto), akiteta jambo na wajumbe wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa ili kurahisisha utendaji kazi wa jumuia hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu na Angelina Malembeka.
 Wajumbe wa Kamati ya Afya, Maafa na Mangira wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Ali Said, Josephat Kadiya na Dk. Meshack Sabaya.

 Wajumbe  wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Omar Njate, Seleman Kumchaya na Seleman Nduda.
Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Mapambo na Makazi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Janeth Sondoka, Amina Mlewa na Khadija Kingi.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wajumbe wa Kamati ya Elimu na Malezi wakifurahia jambo. Kutoka kulia ni Amina Mtemvu, Levocatus Machage, Maria Ernesti na Galila Ramadhan.
Wajumbe wakiwa katika uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages