Breaking News

Your Ad Spot

Nov 27, 2014

KINANA ATINGA WILAYA YA TANDAHIMBA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea maghala ya kuhifadhia korosho wilayani Tandahimba, Mtwara wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi na kupkea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Kinana akisaidia kumtwisha gunia la korosho mmoja wa wapagazi wa maghala ya kuhifadhia korosho, wilayani Tandahimba leo.

 Kinana akikagua mradi wa maji wa Mkupete katika Kata ya Mahuta.

 Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Mdimba, wilayani Tandahimba

 WANANCHI wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika Kata ya Mahuta, wilayani Tandahimba

 Kinana akitembelea baadhi ya nyumba 100 zilizoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa katika Kijiji cha Nanyanda, wilayani Tandahimba

Kinana akiwafariji baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nanyanda ambao wameathirika baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo wa mvua
 Kinana akiendelea kukagua nyumba hizo zilizoezuliwa

 Kinana akipandisha bendera katika Shina la CCM la wakereketwa mjini Tandahimba leo

 Kwaya ikitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Tandahimba

Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Tandahimba, Jaffari Hassan ambaye amehamia CCM,  akielezea sababu zilizosababisha ahamie chama hicho wakati wa mkutano wa hadhara, mjini Tandahimba.Hassan hivi sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa wilaya hiyo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wa Kata ya Kitama akipongezwa na Kinana baada ya kuhamia CCM katika mkutano huo wa hadhara. Hivi sasa ni Mkobo ni Green Guard wa CCM Wilaya ya Tandahimba



 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa
hadhara mjini Tandahimba ambapo alimtaka Katibu Mkuu wa CUF, Seif
Shariff Hamad aache kuwahadaa wananchi kwamba wasiipigie kura Katiba
inayopendekezwa akidai ni ya CCM na kwamba akitaka kuwa mkweli aachie
ngazi nafasi ya Umakamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya
CCM inayoongozwa na CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara, ambapo ameahidi kukutana wadau na viongozi wa mikoa ya inayolima korosho nchini, ili wajadili kero mbalimbali za wakulima wa zao hilo na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, akielezea utekelezji wa miradi mbalimbali jimboni humo wakati wa mkutano huo wa hadhara.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages