Breaking News

Your Ad Spot

Nov 14, 2014

KINANA KUANZA KESHO ZIARA YA SIKU 16 LINDI NA MTWARA

Baada ya kumaliza kwa mafanikio makubwa ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM katika mikoa ya Pwani, Tanga na Iringa hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kesho ataanza ziara kama hiyo ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo jijini Dar es Salaam, kwambam ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu Taifa katika mikoa mbali mbali nchini kwa ajili ya kukagua na kuhimiza uhai wa chama na pia kusimamia utekelezazaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015.

Ifuatayo ni taarifa rasmi kama ilivyotolewa na Nape leo, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,CCM Ofisi ndogo Lumumba.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages