Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa
mazishi ya aliyekuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki jana, yatafanyika kesho
alasiri katika makaburi ya Sinza, Dar es Salaam. Tunaomba tushirikiane katika
kuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, ambapo sekreterieti ya TASWA imemteua Majuto
Omary ambaye ni Mwenyekiti wa TASWA FC, Mwani
Nyangassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Zena Chande Mhazini
Msaidizi kusimamia michango mbalimbali kutoka
kwa waandishi wa habari za michezo nchini kwa ajili ya msiba huo.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/11/2014
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269