Breaking News

Your Ad Spot

Dec 9, 2014

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA UWANJA WA UHURU LEO

Amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akiingia kwa gari maalum kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo, kuongoza maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
Mamia ya wananchi wakiwa wamehudhuria sherehe za maadhimisho hayo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Rais Kikwete akikagua gwaride maalum la maadhimisho hayo
Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein wakiwa wamesimama na viongozi wengine wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Jenerali Devis Mwamunyange
Rais Kikwete akimsalimia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati wa sherehe za maadhimisho hayo. Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe hizo
Baadhi ya mabalozi wa nchi za nje wakiwa kwenye sherehe hizo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages