Breaking News

Your Ad Spot

Jan 8, 2015

MTEMVU APOKEA UGENI KUTOKA VYUO VIKUU VYA MAREKANI

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (katikati mwenye kofia)  akiwa na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Bufalo na Empire vya Marekani baada ya kuwapokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo. Wanafunzi hao wamewasili nchini kwa mwaliko wa mbunge huyo ambapo watatembea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo Job Centre Agency LTD. Wageni hao watapata fursa ya kutembelea jimbo la Temeke, Rolya, Tarime, Kilimanjaro na Mara ambapo watajifunza mambo kadhaa na wataondoka nchini Januari 21, 2015. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
 Mbunge Mtemvu kulia, akielekeza jambo.

Khamisi Mussa

WANAFUNZI 10 kutoka vyuo Vikuu vya Bufalo na Empire vya Marekani wamewasili nchini kwa ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu.

 Akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo mara baada ya kuwapokea wanafunzi hao ambao wanaongozwa na Profesa Dan Nyaronga, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu alisema wageni hao watapata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali iliyopo katika Jimbo lake pamoja na Kampuni yake ya Bravo Job Centre Agency Ltd.

Alisema mbali ya kutembelea jimbo la Temeke pia watatembea Taasisi ya Wajasiriamali ya Poverty Fighting Tanzania iliyopo Tandika na mkoa wa Mara, katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kitenga ambayo waliichangia sh.milioni 1.5, Miradi ya Maendeleo ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime Magharibi, Shule ya Bohare Community Development na Hospitali ya Mkoa wa Mara ambapo watajifunza masuala ya afya.

Alisema baada ya ziara ya mkoa wa Mara watatembelea mkoa wa Kilimanjaro na mbuga za wanyama na kuwa wataondoka nchini Januari 21, 2015.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages