Breaking News

Your Ad Spot

Jan 10, 2015

RIDHIWANI AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHALINZE


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Muumini wa Dini ya Kikiristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.

 Dok Rtaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.

 Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance

 Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa

 Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo

 Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo

 Ridhiwani  pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji  Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula

 Ridhiwani 9katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.

 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza

 Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo

 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo

 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze leo

 Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma, Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati

Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages