Breaking News

Your Ad Spot

Jan 31, 2015

WAKULIMA WA PARETO WASAIDIWA MBEGU NA MICHE YA ZAIDI YA SH. MILIONI 40 NA KIWANDA CHA PARETO (PCT)


 Meneja wa kiwanda cha pareto mafinga (PCT) Martine Oweka


 mkulima akiwa shambani akiendelea kufanya kazi shambani.hili ni shamba lilopo mbeya


 wakulima wakiwa shambani wakiendelea kufanya kazi shambani huko mbeya.


 hii ndio pareto yenyewe ikiwa tayari kwa kuvunwa


naTumaini Msowoya,iringa



KIWANDA cha Pareto (PCT), cha Mafinga wilayani Mufindi kimetumia zaidi ya shilingi milioni 400, kwa ajili ya kuwasaidia wakulima mbegu na miche ya zao hilo, ili kukuza na kuinua zao hilo.




Kila msimu wa Kilimo, kiwanda hicho kimekuwa kikisambaza mbegu na miche ya Pareto kwa wakulima wa zao hilo katika mikoa yote ambayo zao hilo limekuwa likistawi ikiwemo Iringa, Mbeya, Njombe na Arusha.




Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa kiwanda hicho Martine Oweka alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha zao la Pareto ambalo ni mkombozi kwa mkulima.




Oweka amewataka wakulima wa mikoa hiyo  kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kuinua kipato chao na kuondokana na umaskini kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao hilo, tofauti na miaka ya nyuma kufuatia uwepo wa kiwanda.


Oweka alisema ili wakulima waondokane na umaskini, lazima wajikite katika mazao ya biashara likiwemo pareto, kutokana na zao hilo kwa sasa kuwa na bei nzuri katika soko la dunia.


 Alisema kuwa endapo wakulima wa mkoa wa Iringa na mingine inayostawisha zao hilo wataamua kulima pareto kama zao mama la biashara wanaweza kuondokana na umaskini, kutokana na ukweli kwamba, zoko la pareto limekuwa na uhakika tofauti na miaka ya nyuma wakati soko la zao hilo lilipoyumba.


Aliongeza kuwa kwa sasa kiwanda chao kinalima  zaidi ya ekari 300 za pareto, na kwamba kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa wakulima wanalima zao hilo na kufuatilia hatua zote za kupanda, kuvuna, kukausha na kusafirisha hadi kiwandani.

Akizungumzia masoko ya kimataifa Oweka alisema kuwa kwa sasa zipo nchi nyingi ambazo zinauhitaji mkubwa wa zao la pareto na ndiyo maana bei yake ipo juu.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Japani, India, Australia na nchi zilizopo bara la Ulaya kuwa wananunua pareto kwa wingi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages