Breaking News

Your Ad Spot

Feb 21, 2015

HONGERA MILLARD AYO : KUFUNGUA KITUO CHA KURUSHA MAWIMBI YA REDIO


Mtangazaji wako wa nguvu,Millard Ayo mfanyakazi wa Clouds Fm kipindi cha Amplifier amefungua studio kubwa ya kisasa iliyomghalimu mamilioni ya shilingi."Ilikuwa si kazi ndogo kuanzisha hii studio ambayo nimeijenga mwaka mmoja kwa kudunduliza kihasi kidogo kidogo ninachokipata" alisema Millard Ayo.

Ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa Facebook:

"Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini hii na baadae watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa ‪#‎TZA‬ !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa"

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages