Breaking News

Your Ad Spot

Feb 1, 2015

KIKWETE AONGOZA KWA KISHINDO SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 38 YA CCM MJINI SONGEA LEO





 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi alipowasili katika Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, kuongoza sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM kitaifa, kwenye Uwanja huo leo. Rais Kikwete ameongoza sherehe hizo ikiwa ni mara ya mwisho kwake akiwa Rais.
 Wananchi wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipowasili kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 38 ya CCM.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda akikmkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kukagua gwarige maalum lililoandaliwa na Chipukizi wa CCM kwenye maadhimisho hayo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipewa saluti ya heshima na Chipukizi wa CCM baada ya kuvishwa skafu alipoowasili kwenye sherehe hizo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongozwa na Sixtus Mapunda wakati wakipita katika ti ya Chipukizi wa CCM waliomkaribisha na kumisha skafu kwenye sherehe hizo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisherehesha hatua mbalimbali za kufuatwa kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipokea salam za heshima kutoka kwa Chipukizi wa CCM walimwandalia gwaride maalum la sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongozwa na Kamanda wa Gwaride la Chipukizi kwenda kukagua gwaride lililoandaliwa na Chipukizi wa CCM kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride maalum la Chipukizi wa CCM wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipokea salam za heshima kutoka kwa gwaride la Chipukizi wa CCM wakati wa gwaride lililochezwa na Chipukizi wakati wa sherehe hizo za miaka 38 ya CCM. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula
 Kikosi cha bendera cha Chipukizi wa CCM kikipita kwa ukakamavu mbele ya Mwenyekkiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa na Chipukizi hao kusherehekea miaka 38 ya CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea leo
 Chipukizi wa CCM wakitoa heshima kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride hilo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifurahia salam za heshima za Chipukizi wakati wa gwaride hilo.
 Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wao wakati wa gwaride hilo
 "Makomandoo' wa Chipukizi wa CCM wakionyesha uhodari wao mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa sherehe hizo
 'Makomandoo' wa Chipukizi wa CCM wakionyesha ukakamavu wao mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
 'Makomandoo' wa Chipukizi wa CCM wakionyesha umahiri wao katika mapigano ya Kung fu mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa sherehe hizo
 Chipukizi wa CCM wakicheza halaiki ya miaka 38 ya CCM wakati wa sherehe hizo
 Bras Band ya Vijana wa CCM kutoka Zanzibar walioongoza gwaride la Chipukizi wa CCM kwenye sherehe hizo, wakiondoka Uwanjani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Dk. Emmanuel Nchini akitoa maelezo ya utangulizi, kabla ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzungumza kwenye sherehe hizo leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipokea wanachama wapya wa CCM mwishoni mwa sherehe hizo za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, leo. Zaidi ya wanachama wapya 300 wakiwemo kutoka vyama vya upinzani walikabidhiwa kadi za CCM na Kikwete. Kulia ni Mratibu wa Sherehe za Maadhimisho hayo ya miaka 38 ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimuongoza muasisi wa Tanu na baadaye CCM alipowasili kwenye sherehe hizo leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi alipowasili kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe hizo
 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira akilakiwa na Nape alipowasili kwenye sherehe hizo
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Dk. Emmanuel John Nchimbi, akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye sherehe hizo katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Hawa Ghasia
 Msanii wa TOT Plus, Juakali akionyesha vimbwanga vyake kuchangamsha wananchi waliohudhuria kwenye sherehe hizo
Waziri w Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM, Dk. Emmanuel John Nchimbi (kulia) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kushiriki sherehe hizo leo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho.
 Mbunge wa Monduli, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akisalimia wananchi alipowasili kwenye sherehe hizo
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe hizo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Uwanjani, Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi alipowasili kwenye sherehe hizo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Uwanjani, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipowasili kwenye sherehe hizo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Mangula kwenye sherehe hizo
 Baadhi ya wadau wakiwa kwenye jukwaa kuu wakati wa sherehe hizo
 Mkereketwa wa CCM akiwa amejinakshi kwa rangi za CCM na kuwa moja ya burudani kwenye sherehe hizo
 Vijana wa CCM wakifanya amsha amsha kuzunguka Uwanjani mwanzoni mwa shamrashamra za sherehe hizo
 Ofisa kutoka Makao Makuu ya CCM Nyachia alikuwa miongoni mwa washereheshaji katika sherehe hizo
 "CCM Hoyeeee", Mzee Khalfani Mapunda mwenye umri wa miaka 81, akisema wakati wa shamrashamra za sherehe hizo
 Nasibu Abdul aka Diamond Platnam, akiingia uwanja wa Maji Maji kuchangamsha zaidi sherehe hizo
Diamond 'akiwasha moto' na kupagawisha wananchi waliohudhuria kwenye sherehe hizo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages