Breaking News

Your Ad Spot

Feb 20, 2015

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (THBUB) YASIKITISHWA NA MAUAJI YA MTOTO YOHANA BAHATI



Celina Mathew

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inesikitishwa na mauaji ya kikatili ya mtoto Yohana Bahati aliyetekwa nyara hivi karibuni katika kijiji cha Ilemela, Chato Mkoani Geita.

Aidha, tume hiyo inaungana na wananchi, wadaumablimbali na Serikali kulaani mauaji ya mtoto huyo na kujeruhuwa vibaya mama yake wakati akitetea haki ya mwanaye kuishi katika jamii huru, na inakemea vikali vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga alisema tume hiyo inawakumbusha wananchi kuwa vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi ni matukio ya ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu.

"Matukio haya yanaonesha yamekua yakichangiwa na imani za kishirikina hivyo tume inakemea matendo haya na kutaka yapigwe vita,"aliseama.

Aliongeza chini ya katiba na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu serikali ina wajibu wa kulinda raia wake hivyo tume hiyo imeitaka serikali kuwasaka waliohusika na vitendo hivyo na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

"Tume inakumbusha serikali kuwa wakati umefika wa kufanyia marekebisho makubwa sheria ya uchawi (sura ya 18 ya 1928) au kutunga sheria mpya ili kupiga marufuku vitendo vinavyoendeleza imani za uchawi na ushirikina, pia ipitie upya sheria inayowatambua waganga wa jadi (sheria ya tiba asili na Tiba Mbadala)"alisema.

Aidha, tume hiyo inatoa mwito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kuachana na imani potofu zenye mtizamo hasi kwamba mafanikio yoyote yanaweza kupatikana kwa njia za kishirikina bali yanapatikana kwa kufanya kazi halali kwa bidii na siyo njia za kishirikina ikiwemo kutumia viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.

"Tume ipo mbioni kwa kushirikiana na wadau wengine kutekeleza mpango wa kitaifa wa kuelimisha wananchi ili kuepusha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini hivyo wananchi tushirikiane katika hilo,"alisema.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages