Pamoja na kukataa kwamba hakumtemea mate mshambuliaji wa New Castle Papis Cisse, beki wa Man United, Jonny Evans amefungiwa mechi sita na Shirikisho la soka England FA. Naye Papis Cisse amefungiwa michezo saba na Shirikisho hilo.
FA
imetoa adhabu hiyo baada ya kuthibitishwa kupitia mkanda wa video ya mchezo uliochezwa Jumatano iliyopita katika uwanja wa St. James Park ambapo Man U waliibuka na ushindi wa goli 1-0, goli lililofungwa na Ashley Young.
Adhabu
hiyo itamfanya beki huyo kukosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Arsenal
siku ya jumatatu kwmenye uwanja wa Old Tranford na michezo mingine
atakayoikosa ni ile dhidi ya Tottenham, Liverpool, Aston Villa, Manchester City, na Chelsea. Kwa upande wa Cisse atakosa michezo dhidi ya Everton, Arsenal, Sunderland, Liverpool, Tottenham,Swansea na Leicester
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269