Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2015

CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA MAFUNZO YA WATAALAMU WA TAKWIMU NA CHUO CHA TAKWIMU CHA INDIA

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kukamilika kwa maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. (Picha zote na Veronica Kazimoto) 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiwaelezea Waandishi wa Habari jinsi alivyofurahishwa na maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akimsalimia mwanafunzi wa Udhamili katika Takwimu Rasmi Happiness Katuma wakati akikagua baadhi ya vitu  mbalimbali kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akipitishwa katika maeneo mbalimbali ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kama maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa chuo hicho na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akisoma moja ya vitabu kilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akimwelezea Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.

Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam,
17 Machi, 2015.
CHUO cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimekamilisha maadalizi ya kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha EASTC Prof. Innocent Ngalinda amesema mkataba huo utasainiwa tarehe 28 Machi, 2015.
 
“Maandalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu na Chuo cha Takwimu cha nchini India yamekamilika kwa kiasi kikubwa na ndio maana hapa mbele yenu mnamuona Naibu Balozi wa Ubalozi wa India hapa nchini amefika kwa ajili ya kujirizisha”, amesema Prof. Ngalinda.
 
Prof. Ngalinda amesema kuwa mkataba huo una manufaa makubwa kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa wataalam wengi katika tasnia ya takwimu hapa nchini.
Pamoja na ongezeko la watalaam wa takwimu hasa wakufunzi, kutakuwa na ukarabati wa miundombinu katika chuo hicho ambapo mabweni ya wanafunzi pamoja na ofisi za chuo hicho zitakarabatiwa.
 
Prof. Innocent Ngalinda amefafanua kuwa katika mkataba huo, kutakuwa na mpango wa kubadilishana wanafunzi katika vyuo hivyo viwili ili kupanua uelewa wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi zaidi katika masuala ya kitakwimu.
 
Kwa upande wake Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal amefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika na kusema kuwa nchi yake iko tayari kutiliana saini ya mkataba wa makubaliano ya mafunzo ya Watalaam wa Takwimu kutoka chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na chuo cha Takwimu cha nchini India.
 
“Nimefurahishwa na maandalizi yaliyofanyika katika chuo hiki na sasa tunamsubiri Waziri wa mambo ya Nje wa nchini India kwa ajili ya kutiliana saini ya mkataba huu ifikapo tarehe 28 Machi, 2015,” amesema Naibu Balozi Humpal.
 
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam na chuo cha Takwimu cha India vimekuwa vikishirikiana tangu mwaka 2012 lakini ushirikiano huo haukuwa rasmi hivyo vyuo hivyo vimeamua kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili kufanya ushirikiano huo kuwa rasmi.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages