Breaking News

Your Ad Spot

Mar 28, 2015

JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA DAR ES SALAAM YAFANYA SEMINA KUHUSU KATIBA ILIYOPENDEKEZWA

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni Mwinyimkuu Sangaraza (kushoto), akizungumza na wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho wa Mkoa wa Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa Semina ya siku moja kuhusu katiba iliyopendekezwa. Wilaya ya Kinondoni ilikuwa ni mwenyeji wa semina hiyo.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Cholaje Ali (kulia), akizungumza na wajumbe wa jumuiya hiyo wakati akitoa maelekezo ya ugawaji vifaa mbalimbali kwa wajumbe wa wilaya hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Khadija Hassan Mzee na katikati ni Diwani wa Kata ya Ndugumbi ambaye pia ni Mwenyekiti wa jumuiya hiyo wilaya ya Kinondoni, Lucas Mgonja.
 Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.
 Makada wa CCM wakiwa kwenye semina hiyo.
 Wajumbe wa jumuiya hiyo wakiwa kwenye semina hiyo.

 Ndoo za plastiki zilizokuwa na jagi, vikombe na sahani zilizogaiwa kwa wajumbe hao. Mbali na ndoa hizo wajumbe hao walikabidhiwa skafu, fulana na vitenge.
 Mabeseni waliyokabidhiwa wajumbe wa jumuiya hiyo 
wa wilaya hiyo.
Viongozi wa jumuiya hiyo wa Kata ya Kwembe wakisubiri kukabidhiwa vitu hivyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages