Breaking News

Your Ad Spot

Mar 14, 2015

DR. SLAA KUTINGA KORTINI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MLIZI WAKE


JESHI la Polsi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lipo katika hatua ya mwisho katika kukamilisha ushahidi ili kumfikikisha mahakamani Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dokta Wilbrod Slaa pamoja na makada wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana mchana Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam Suleiman Kova alitaja sababu ya kumfikisha mahakani katibu huyo wa CHADEMA na makada wake kuwa ni vitendo vinavyodaiwa ni vya kinyama alivyofanyiwa mlinzi wake vya kumteka, kumpiga na kumlazimisha kutaja watu wanaomtuma kumuua Dr.Slaa
 
Jeshi hilo  limesema kwa sasa linawashikilia makada watatu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini ambao ni Boniface Jacob (miaka 32) mkazi wa Ubungo Kisiwani ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ubungo kupitia chama hicho, Hemed Ally Sabula (miaka 48) mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambaye anadaiwa ni Afisa Usalama wa chama hicho Taifa.

Mbali na hao pia Kamishna Kova alimtaja kada mwingine anayeshikiliwa kuwa ni Benson Mramba (miaka 30), mkazi Tabata Kisukulu ambaye ni Afisa Utawala wa CHADEMA.

Kamishna Kova alibainisha kuwa ushahidi wao utakapokamilika mafaili yao yatafikishwa kwa Wakili wa Serikali ili hatua zichukuliwe. 

Akizungumzia sakata la mlinzi Kagenzi, Kova alisema kuwa kwa sasa wanamalizia kazi ya kukusanya ushahidi kutoka CHADEMA ambao wanamtuhumu bwana Kagenzi ambaye anafanya ushirikiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni kuandaa mpango wa kutaka kumuwekea sumu Dokta Slaa.

Kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilifika Polisi tarehe 8 mwezi huu majira ya saa 11 jioni katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kupitia kwa wakili wa CHADEMA anayetambulika kwa jina la john Mallya akiambatana na mtuhumiwa Khalid Kagenzi ambaye ni mkazi wa Tandale kwa Tumbo ambapo Wakili huyo aliiambia polisi kwamba alimleta mtuhumiwa baada ya kuagizwa na Dokta Slaa ili kutoa malalamiko kwa niaba yake.

Katika maelezo yake anadai Wakili huyo kuwa uongozi wa CHADEMA ulikuwa umechukuwa hatua mbalimbali dhidi ya Kagenzi ikiwemo kumbana na kujiridhisha kuwa anahusika na mipango ya kimauaji.

Kwa mujibu wa Kamishna Kova, katika mahojiano walibaini kuna vitendo vya kinyama ambavyo mlinzi huyo wa Dokta Slaa amefanyiwa na makada wa CHADEMA baada ya Jeshi hilo kumkuta akiwa na majeraha mbalimbali katika mwili wake.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages