Breaking News

Your Ad Spot

Mar 16, 2015

KINANA AAHIDI KUTAFUTA UFUMBUZI WA KUDUMU MGOGORO WA MIPAKA MBUGA YA NGORONGORO NA WANANCHI

Akijibu hoja zao Ndugu Abdulrahman Kinana amesema hawezi kujibu lolote kwa sasa ili asije kuonekana amedanganya. lakini ameahidi kurudi kijijini hapo baada ya mwezi mmoja mara baada ya kukutana na Mawaziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na kupata taarifa juu ya ahadi ya Waziri Mkuu pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na mhifadhi wa Ngorongoro ili kuzungumzia suala hilo kwa ajili ya kupata ufunbuzi wa kudumu.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NGORONGORO-ARUSHA) 2Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukisalimiana na Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro Consevation Area Authority Bw. Bruno Kawasange mara baada ya kuwasili katika katika ofisi hizo kwa ajili ya kuzungumza na baraza la wafugaji, Wazee wa kimila na viongozi wa kata. 3Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya asili ya watu wa kabila la Wabarbaigi iliyokuwa ikitumbuizwa wakati wa mapokezi yake.  4Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano uliomkutanisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Baraza la Wafugaji, Viongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Wazee wa kimila. 5Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza katika mkutano huo. 6Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Bulati. 7Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge wa jimbo la Ngorongoro na naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Saning’o Ole Telele wakishiriki kupaka rangi kwenye nyumba ya mganga wa zahanati ya kijiji cha Bulati 9Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Nape Nnauye wakiondoka mara baada ya kushiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho cha Bulati. 10Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Nainokanoka 11 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia Kikundi cha Ngoma kilipokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi yawakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Nainokanoka 12 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika kijiji cha Nainokanoka. 13 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, 14Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Daudi Felix Ntibenda akiwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nai 15Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji Nainokanoka. 16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mbuzi waliokabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya kata ya Nainokanoka. 18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika zoezi la kuhesabu mbuzi waliokuwa wakikabidhiwa kwa vikundi hivyo. 19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi buzi hao kwa vikundi mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages