Breaking News

Your Ad Spot

Mar 19, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA SHEREHE YA KUTIMIZA MWAKA VIKUNDI VYA WAMA HUKO NACHINGWEA/ AKABIDHI MADAWATI

1Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Chuo cha Ualimu Nachingwea kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe 18.3.2015.
2Mamia ya wanavikundi na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika Mkoa wa Lindi zilizofanyika Nachingwea wakifuatilia kwa makini sherehe hiyo.
3 4Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaonyesha waalikwa zawadi mbalimbali alizopewa na wanavikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe mkoani Lindi. Sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Elimu Nachingwea tarehe 18.3.2015 7Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wana vikundi vya WAMA katika Mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi hivyo zilizofanyika Nachingwea tarehe 18.3.2015.
10Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akimkabidhi cheti kwa Bi Fatuma Mchia, Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya WAMA Kwenye Mradi wa Mwanamke Mwezeshe kwa kuvuka lengo kwa kuingiza wanavikundi wengi kwenye mradi huo.
11Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akianzisha mchango wa papo kwa papo kwa ajili ya Mradi wa Mwanamke Mwezeshe na kufanikiwsa kukusanya zaidi ya shilingi milioni moja.
12Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachuo wanaosomea ualimu kwenye Chuo cha Ualimu Nachingwea mara baada ya kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe zilizofanyia chuoni hapo tarehe 18.3.2015.
14Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akishiriki katika mkutano wa ndani wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa akitokes Nachingwea ambako alihudhuria sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi vya WAMA kwenye mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe b18.3.2015.
16Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM,Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa ambao walijikusanya kwa wingi hadi kupelekea Mama Salma kusimama na kuzungumza nao. Mama Salma Kikwete yupo mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
17Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimia mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mnacho iliyoko wilayani Ruangwa. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kukabidhi madawati 100 aliyowaahidi wakati alipozuru shule hiyo mwaka jana.
18Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikabidhi madawati 100 kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Ndugu Sahius Kilowoko (kushoto) ambaye naye alimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Nicholaus Kombe (kulia). Mama Salma alitoa madawati hayo kwa Shule ya Msingi Mnacho iliyoko wilayani `humo tarehe 18.3.2015.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages