Breaking News

Your Ad Spot

Mar 28, 2015

MCHUNGAJI GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI KUHOJIWA JUU YA LUGHA CHAFU DHIDI YA ASKOFU PENGO


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo. 
 
Matusi hayo   ni  yale yaliyoonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii  ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.

Hata  hivyo, mapema  leo  Asubuhi, kipande cha  sauti   ya  Gwajima kilisambaa   katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii  kikidai kuwa Gwajima angejisalimisha Polisi Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu.

Haijafahamika  mara  moja  sababu  zilizomfanya  mchungaji  huyo  Kujisalimisha  leo  Ijumaa.

Nimekuwekea  Kipande  hicho  hapo  chini  ambapo  Gwajima  anajitetea  ni  kwa  nini  Alitumia  lugha  hiyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages