KESI
za kulawiti watoto mashuleni imeelezwa kuwa wanaofanya ukatili huo wa
kijinsia kwa watoto hao baadhi yao ni walimu wanaowafundisha na kwamba
kutokana na walimu hao kuhitajika shuleni hapo baadhi ya uongozi wa
shule umekuwa ukishindwa kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kushindwa
kuripoti katika dawati hilo.
Mkaguzi
Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoani
Kilimanjaro Prisca Maganga aliwaambia waandishi wa habari wa mikoa ya
Manyara, Tanga, Kilimanjaro na Arusha waliotembelea dawati hilo mwishoni
mwa wiki kuwa kwa mwezi Januari hadi Februari mwaka huu wamepokea kesi
10 za kutelekeza familia zikiwemo kesi 2 za kubaka.
Alisema
kesi mbili hadi tatu za kulawiti wanafunzi wa shule za msingi mkoani
Kilimanjaro zimeripotiwa kwa mwezi Januari hadi Februari mwaka huu
katika dawati la jinsia mkoani humo ambapo katika kesi 10 zilizoripotiwa
katika dawati hilo zilikuwa zikiongozwa na kesi za kutelekeza familia.
“Kesi
za ukatili wa majumbani kama kutelekeza familia zinaongoza kwa mkoa
wetu, tunapokea kesi 10 hadi 15 kwa mwezi chimbuko likiwa ni kiuchumi na
changamoto za maisha na akinamama wengi wanatelekezwa kwa sababu ya
utegemezi na sababu nyingine wanaume kuwa na tamaa na kuoa mke
mwingine,” Alisema mkaguzi huyo wa Polisi.
Akielezea
ukatili mwingine wa majumbani, alisema wazazi wengi wamekuwa wakitoa
adhabu za viboko na vipigo vinavyokithiri kwa watoto wao kwa lengo la
kuwakanya kitabia bila kujua kwamba zipo sheria zinazomlinda mtoto huyo
dhidi ya ukatili huo na wakati mwingine wazazi hao kulazimika kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
“Baba
mmoja alikuwa akimpiga mtoto wake kwa mjeledi na kuacha alama mbaya
mwilini mara kwa mara na kuathiri masomo na makuzi yake na kumpiga mama
wa mtoto huyo kumbe wazazi hao ni waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi,
tunashukuru walimu wa shule aliyokuwa akisoma mtoto huyo kutupa taarifa
na ushirikiano hadi mtoto huyo kuendelea na masomo yake mpaka sasa,”
alisema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269