Wakati joto la mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, itakayopigwa leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, likiwa juu kadiri inavyokaribia kipute hicho kuanza saa kumi jioni hii, swali lililopo katika kila shabiki wa soka nchini na duniani kote ni je timu gani itafanikiwa kuwapaisha mashabiki wake kwa kutoka na ushindi Uwanjani?
Mchezo huo utakaochezeshwa na Mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Soud Lila kutoka Dar es Salaam, mshika kibendera wa kwanza, Florentina Zabron (Dodoma) mshika kibendera wa pili, Mwamuzi wa akiba ni Israel Mjuni, na kamisaa wa mchezo ni Ame Santimeya wote kutoka Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), viingilio vya mchezo huo, VIP
A sh. 40,000, VIP B sh. 30,000, VIP C sh. 20,000, Rangi ya Machungwa
(Orange) sh. 10,000, huku Rangi ya Bluu na Kijani ikiwa ni sh. 7,000.
Tiketi zilianza kuuzwa jana (jumamosi) saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya, Karume
(Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni),
BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa
Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Magari
yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja siku
ya jumapili kwa kupitia barabara ya Mandela na Uwanja wa Uhuru,
barabara ya Chang’ombe itafungwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi.
TFF
inawaomba, wapenzi, washabiki na wadau wa mchezo kununua tiketi katika
vituo vilivyotajwa ili kuepuka kuuziwa tiketi bandia, ili kuimarisha
ulinzi na usalama wa mchezo, mashabiki wenye mabegi, silaha, vilevi na
chupa za maji hawataruhusiwa kuingia navyo uwanjani.
Aidha,
katika mchezo huo TFF itatoa ujumbe maalum kupitia kwa wachezaji
kuhamasisha juhudi za Taifa za kuzuia mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu
wa ngozi (Albino).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269