Basi la wachezaji wa kano Pillars lililoshambuliwa na wapiganaji nchini Nigeria
Wachezaji
watano wa kilabu ya Kano Pillars nchini Nigeria walipigwa risasi na
wapiganaji katika shambulizi lillolenga msafara wa kilabu hiyo wakati
wachezaji hao walipokuwa wakielekea Owerri katika mechi ya ufunguzi wa
Ligi kuu nchini Nigeria.
''Wachezaji
watano walijeruhiwa kutokana na shambulizi la risasi .Wachezaji hao ni
Gambo,Ogbonaya,Eneji Otekpa na Murtala Adamu'', ulisema ujumbe wa
mtandao wa twitter wa kilabu hiyo.
Wapiganaji hao pia walichukua simu pamoja na vitu vyengine muhimu vya wachezaji hao.
kano Pillar
Mechi iliokuwa ichezwe siku ya jumamosi kati ya timu hiyo na ile ya Heartland imeahirishwa mara moja.
Kilabu
hiyo ya Kano Piilars ilikuwa ndani ya basi lililowabeba wachezaji
25,ikiwemo wachezaji 18,wakati wa tukio hilo lililotokea mwendo wa saa
saba na robo saa za Nigeria.
kano Pillars
Wachezaji waliojeruhiwa kwa sasa wanaendelea kupokea matibabu katika kituo cha matibabu cha Lokoja.
Siku
ya ijumaa beki wa kilabu hiyo Reuben Ogbonnaya aliiambia BBC kwamba
anamshukuru Mungu kwa kumuezesha kuishi kwa sababu hajui ni nini
kingetokea.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269