Hali
ya taharuki imetanda katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha baada ya
kugundulika mahali walipofichwa watoto 17 wakiwamo watatu wa familia
moja wanaodaiwa kupotea tangu mwezi Februari mwaka jana kwa madai ya
kufundishwa maadili ya imani ya dini ya kiislamu.
Umati
mkubwa wa wakazi wa mji wa Moshi wamejitokeza katika kata ya Pasua
mjini Moshi kushuhudia tukio la watoto hao wenye umri wa kuanzia miaka
miwili hadi 13 ambao walikuwa wanaishi kwa Bw.Abdelnasir Abrahamani
ambaye ni mfanyabiashara wa nguo nchini Kenya.
Akizungumza
katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Moshi Bw.Novatus Makunga amesema
tatizo hilo kwa mji wa Moshi ni kubwa na kwamba kwa sasa nyumba hiyo
imefungwa na kuondolewa watoto hao ili warejeshwe kwa wazazi hao wakati
hatua za kisheria zikiendelea.
Mmoja
wa wazazi mwenye watoto watatu waliopotea tangu mwezi February mwaka
jana na kukutwa katika nyumba hiyo Bw.Ramadhani Mohamedi amesema
aligundua tukio hilo baada ya kukutana na mtoto wake wa kike barabarani
na kumweleza mateso wanayoyapata huko.
Naye
mfanyabiashara huyo Bw.Abdulinasir Abrahamani amesema nyumba hiyo ni
familia na ndugu zao wa kiislamu lakini siyo kituo cha yatima, ila ni
sehemu ya kutolea mafundisho ya dini ya kiislamu.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269