Jeshi
la polisi mkoa wa Mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili
wa Serikali ya kijiji cha Park Nyigoti katika kata ya Ikoma wilayani
Serengeti mkoani Mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga
vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa
viboko na kusababisha vifo vya watu watano.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Mara,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi
ACP Ernest Kimola,amesema katika tukio hilo limesababisha watu
wengine watatu kujeruhiwa na viboko hivyo na kulazwa katika hospitali
teule ya Nyerere DDH Mjini Mugumu wilayani Serengeti.
Amesema
mbali na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya kijiji kukamatwa pia
viongozi wawili wa jadi wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.
Amesema kabla ya kuwakamata wananchi hao wakiwa katika miji yao kisha kuwafunga vitambaa usoni na kuwachapa viboko hadi kufa kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya ushirikina,viongozi hao jadi kwa kushirikiana na Serikali ya kijiji waliitisha mkutano kwa lengo la kuwabaini watu wanajihusisha na ushirikiana ambao umesababisha mvua kutonyesha kijijini hapo ambapo watu wanane walitajwa katika mkutano huo.
Kaimu
kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara,amewataja waliouawa katika tukio
hilo lililotokea alfajiri ya tarehe 2.3.2015 kisha miili yao kutupwa
karibu na miji yao kuwa ni Nyahita Nyambeho,Nyasari Holela,Joseph
Msoba,Nyangi Nyakitambara na Nyangi Kanyaro wote wakazi wa kijiji
hicho ambapo Raphael Holela,Masenze Nyamsero na Elizabeth Mwita
wamelazwa katika hospitali ya Nyerere DDH baada ya kuchapwa viboko na
kujeruhiwa vibaya.
Hadi
sasa jeshi la polisi kutoka makao makuu ya mkoa wa Mara kwa
kushirikaina na polisi mjini wilayani Serengeti wanaendesha na
operesheni kali katika kuwasaka watu wote walihusika kufanya mauaji hayo
ya kinyama.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269