Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2015

WAZIRI WA MAJI PROFESA MAGHEMBE AZINDUA MAADHIMISHO YA 27 YA WIKI YA MAJI KITAIFA

Waziri wa Maji Profesa Jumanne  Maghembe akiakata utepe kuashiria uzinduzi wa Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa yanayofanyika katika mji wa Musoma mkoani Mara.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne  Maghembe, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Idara ya Maji Vijiji iliyoko Wizara ya Maji wakati akikagua mabanda ya maonesho kwenye shule ya Msingi Mkendo mjini Musoma mkoani Mara.
Mkemia wa Wizara ya Maji Rocho Mkole akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji Prof. Maghembe wakati alipotembelea banda la wizara hiyo.
Mhandisi wa Mazingira wa Idara ya Rasilimaji za Maji kutoka Wizara ya Maji, Eng. Modest Zakari akitoa maelezo kwa Waziri Profesa Maghembe kuhusu kilimo cha umwagiliaji.
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akiangalia kifaa cha kupimia maji kwenye banda ya kampuni ya kampuni ya NFOSYS PS, huku Msambazaji Mkuu wa Wizara Crepi Bulamu na wataalamu wa kampuni hiyo na wakishuhudia. 
Waziri wa Maji Profesa Maghembe akiangalia baadhi ya mitambo ya banda la kampuni ya DPI Simba Limited wakatia akitembelea mabanda.Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Jai Patidar.
Waziri Profesa Maghembe (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Aseri Msangi.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba.
Waziri wa Maji Prof. Maghembe akihutubia wananachi.
Waziri wa Maji Profesa Maghembe, akizungumza na wanahabari.
Kikundi cha burudani kikiburudisha, wakati wa hafla hiyo.
Mwalimu Msomi wa Shule ya Sekondari Kisangula kutoka Wilaya ya Serengeti, akiongoza wimbo wa kuhamasisha kutunza vya nzo vya maji.
Mkuu wa Idara ya Rasilimali za Maji na Uhandisi wa Umwagiliaji wa Chuo cha Maji, Eng. Pantaleo Tumbo akitoa elimu kwa wananchi waliohudhuria kwenye maonesho ya maadhimisho ya wiki ya maji. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO) 

Na Hussein Makame-MAELEZO
ZAIDI ya wananchi Milioni 7 wamepatiwa maji safi na salama katika miji ya mikoa, wilaya na miji midogo nchini kutokana na kuboresha huduma za majisafi na uondoaji majitaka mijini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne  Maghembe wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa yanayofanyika katika shule ya Msingi Mkendo mjini Musoma mkoani Mara.
Prof. Maghembe amesema uboreshaji huo ni kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi katika miji mikuu ya mikoa, wilaya, miji midogo na miradi ya maji ya kitaifa.
AlisemaSerikali kupitia  Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji imejenga miradi mipya 663 imejengwa katika vijiji 10 kwa kila halmashauri nchini na miradi 68 ya upanuzi na ukarabati kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
“Utekelezaji huo umekamilisha miradi 731 iliyopangwa kutekelezwa  na unajumuisha miradi 390 ambayo haikukamilika katika mwaka wa fedha 2013/2014” alisema Prof. Maghembe na kuongeza:
“Kuanzia mwezi Julai 2013 hadi mwezi Desemba 2014, jmla ya miradi ya maji 674 ilijengwa na kukamilika.Idadi hii inatokana na ujezni wa miradi mipya 433 ya vijiji 10 katika kila halmashauri na miradi mingine 241 ya upanuzi na ukarabati”.
Alifafanua kuwa miradi hiyo imevipatia maji vijiji 900 na jumla ya vituo vya kuchotea maji 18610 vilivyojengwa ambavyo vinahudumia watu 4,568,402 na kuanzisha vyombo vya watumia maji 560.
“Usimamizi huo imepelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama vijijini kutoka asilimia 40 Julai 2013 hadi asilimia 53.08 za sasa” alisema Profesa Maghembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kapteni Mstaafu Aseri Msangi aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha kuwa wanapata maji kwa muda wote.
Alikizungumzia hali ya maji Kapteni Mstaafu Msangi alisema kwa sasa upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 46.3 wakati maeneo ya mijini upatikanaji wa maji ni asilimia 53.5.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,  Mhandisi Mbogo Futakamba aliwaasa wananchi, mashirika na wadau wote wa sekta ya maji kuunga mkono jhudi za kuboresha huduma za maji hapa nchini.
Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi watambue kuwa maji ni rasilimali muhimu katika kupiga vita umasikini na kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.
Waziri Prof. Maghembe alisema Madhumuni ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji  ni kuhamasisha, kutoa elimu kwa umma kuhusu Sekta ya Maji na kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mipango ya utunzaji wa rasilimali za maji na uhifadhi wa mazingira.


Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Majiyamebeba Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Maendeleo Endelevu” ambapo yataambatana na uzinduzi au uwekaji mawe ya msingi ya miradi ya maji ikiwemo mradi mkubwa wa Maji wa mji wa Musoma

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages