Breaking News

Your Ad Spot

Apr 3, 2015

IJUE IJUMAA KUU

 Agias_Triados_frescos_cross
Ijumaa Kuu ni siku ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa.
Kadiri ya Mtume Yohane kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.
Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaaniMasiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.
Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake, kulala kaburini, na hatimaye kufufuka kwa utukufu
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.
L_F_Schnorr_von_Carolsfeld_Die_drei_Marien_am_Grab_Jesu
Zinamuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo cha msalaba; siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu; siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu. 
Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages