Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2015

LIGI YA ENGLAND TIMU 20 KUSHUKA DIMBANI

Timu ya Chelsea
Kocha wa Liverpool,Brendan Rodgers
Jumla ya timu 20 zinazoshiriki ligi ya England zinatarajiwa kushuka dimbani mwishoni mwa wiki.
Hata hivyo mechi ya Chelsea na Arsenal ,inaoonekana kuwa na mvuto zaidi kwa wengi, kufuatia matokeo ya mechi hiyo kutoa picha mbili tofauti, moja kuihakikishia Chealse ubingwa iwapo itashinda mechi hiyo,na pia Arsenal ikishinda italeta mazingira ya wazi kwa timu yoyote kati ya timu hizo mbili kutwaa ubingwa.
Kocha wa Liverpool,Brendan RodgersNaye kocha Liverpool Brendan Rodgers ameibuka na kutamba kuwa yeye ni kocha bora na hakuna kama yeye, huku akisema anamatumaini ya kuendelea kukinoa kikosi.
Pamoja na majigambo hayo Rodgers ameweka rekodi mpya ndani ya klabu hiyo kwa kuongoza misimu mitatu bila kuchukua taji lolote, tofauti na watangulizi wake tangu mwaka 1950

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages