Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2015

URAIS WAZUA TAFRANI BURUNDI, MMOJA AUAWA KATIAK MAANDAMANO MJINI BUJUMBURA


Ghasia zazuka nchini Burundi
Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi.
Waandamanaji wameishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa.
Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages