Waandamanaji wakiwa Mjini Bujumbura.
Kumezuka
ghasia katika Mji wa Bujumbura nchini Burundi kati ya maofisa wa polisi
na waandamanaji wanaoishutumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya
kikatiba.
Waandamanaji walirusha mawe na kuchoma matairi huku maofisa wa polisi wakilazimika kurusha mabomu ya machozi hewani.
Ghasia
hizo zinafuatia tangazo la jana kwamba Rais wa Burundi, Pierre
Nkurunziza ameteuliwa na chama chake kuwania muhula wa tatu wa urais.
Upinzani
umeitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa katiba na kuonya kuwa huenda
ikaathiri makubuliano ya amani ambayo yalimaliza miaka kadhaa ya
mapigano ya kikabila.
Serikali imesema kuwa maandamano hayo si halali.
Maelfu
ya raia wa Burundi wamelitoroka taifa hilo katika majuma ya hivi
karibuni wakihofia kuongezeka kwa ghasia hizo huku taifa hilo
likijiandaa kwa uchaguzi utakaofanyika Mwezi Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269