Breaking News

Your Ad Spot

Apr 24, 2015

WAANDAMANA KUPINGA UBAGUZI AFRIKA KUSINI



Waandamana dhidi ya ubaguzi
Afrika Kusini

Maelfu ya raia wa Afrika
Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya mashambulizi
dhidi ya raia wa kigeni.

Mikutano mikubwa imeandaliwa
katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa
nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya
kigeni mnamo mwaka 2008.

Makundi ya kiusalama
yanafanya misako katika majumba ya makaazi katika mji wa Alexandra mjini
Johannesburg, mahala ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika
yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.



Mwaandishi wa BBC anasema
kuwa, kuonekana kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages