Katibu wa Chadema Mkoa wa Morogoro Ndugu Samwel Kitwika
…………………………………………………………………
Na Bryceson Mathias, Morogoro.
Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Morogoro, kimejigamba kitakomba Wabune Watano (5),
na Madiwani 16, watakaotimkia Chadema wakidai kuchoshwa na Rushwa
inayofanywa katika mchakato wa kuwania nyadhifa hizo.
Akizungumza na Mwandishi jana,
Katibu wa Chadema Morogoro, Samwel Kitwika, alisema, Rushwa, Ukiritimba
na Mchezo Mchafu uanaoendelea ndani ya CCM Morogoro kuwapata wawakilishi
hao, ndiyo Mtaji na Mvuto, utaowakimbiza CCM na kutaka kutimkia
Chadema.
Alipoulizwa iwapo anaweza kuwataja Wawakilishi hao, Kitwika
alisema,”Kwa sasa hatuwezi kuwataja Wabunge na Madiwani hao, maana ni
sawa na kumuonesha adui mbinu zako, isipokuwa ifahamike wanatoka katika
Majimbo yote 10 ya Mkoa wa Morogoro na Kata zake.
“Sababu kubwa inayotangulia katika kufikia maamuzi hayo, ni
Umaarufu wa Chadema tangu ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya hadi Msingi,
vikiunganisha na Uadilifu na umoja ndani ya Chama, vinavyopelekea,
kudhibiti Rushwa, Ufisadi na Maovu mbalimbali nje na ndani ya
Chama”.alisema Kitwika.
Kitwika aliongeza kwamba, awali walikuwa na madiwani 10
waliofika kwenye ofisi za Chadema kuomba kuungana na Chama kulileta
Taifa ukombozi wa kweli kwa wananchi walioumizwa na Rushwa na Maovu,
lakini wiki hii, wameongezeka Madiwani Sita, na kufanya wafikie 16.
Mmoja wa Madiwani wa Moja ya Kata za Jimbo la Mvomero (Jina
linahifadhiwa) alisema, “Kutokana na Malumbano ya yeye na Chama chake
katika eneo la kufanywa Mhuri (Rubber Stamp) wa kupitisha Maovu,
wanipitishe/Wasinipitishe, naondoka na watu wangu kwenda
Chadema”.alisema Diwani huyo.
Awali Chadema kilimwaga Watia Nia wanaowania Ubunge na
Udiwani katika Majimbo na Kata zinazoshikiliwa na CCM, ambapo waliwasha
Moto wa kutoa Elimu na kuwajengea Uwezo watu, juu ya Nia ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA, kutwa Dola, na kuwaatia Neema.
Aidha mmoja wa Viongozi Wakongwe wa CCM Mkoa wa Morogoro
aliyeomba asitajwe jina gazetini alisema, Kauli ya Chadema ni sawa na
mtu anayeota na kulala usingizi akiwa juu ya Mti, ambapo akidondoka,
hupoteza Maisha yake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269