Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika
Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205.
Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada
ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati
akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015
kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal. Picha na OMR Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati
akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC,
jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015. Picha na OMR
Rais
wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt
Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha
Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa
dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini
Harare, Zimbabwe.
Kufuatia
makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na
matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na
masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya
kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali
Afrika. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269