Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2015

NAPE AHIMIZA MSHIKAMANO JMBO LA MTAMA

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akisalimiana na Mzee Masoud Ali Chitende Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mtama mara baada ya kuwasili kwenye kata ya Mtama ambapo alipata nafasi ya kuwasalimu wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata Mtama na Majengo, Mtama mkoani Lindi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtama Mzee Said H. Maluma,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo Mzee Omari Mataka.
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata ya Mtama na Majengo wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye .
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mtama Mzee Said H. Maluma akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  CCM Taifa Nape Nnauye kwenye ofisi ya CCM kata ya Mtama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata ya Majengo na Mtama mara baada ya kukutana nao na kuwasalimu kwenye ofisi za CCM kata ya Mtama ambapo aliwataka Wajumbe hao na wana CCM wa Mtama kushikamana na kushirikiana katika kila jambo la kujenga na kuimarisha Chama kwani kufanya hivyo Chama kitakuwa imara zaidi Mtama na kila mwana CCM atajivunia mafanikio ya Chama chake.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Yahaya Nawanda akiteta jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakati wa kumsindikiza Katibu wa NEC aliyepita Lindi kwa lengo la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages