Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Singida, wakishiriki maandamano kama sehemu ya
maadhimisho ya sherehe za sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
mwaka huu iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini hapa.(Picha na
Nathaniel Limu).
MKUU
wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, amewaasa watumishi wa umma
kuwa wasiwe wepesi wa kudai haki zao, bali kwanza watimize wajibu wao
kikamilifu kwa madai kwamba haki na wajibu huambatana pamoja.
Dk.Kone
ametoa usia huo wakati akizungumza kwenye kilele cha sherehe za sikukuu
ya wafanyakazi (Mei Mosi) mwaka huu, zilizofanyika kimkoa katika uwanja
wa Namfua mjini hapa.
Alisema
wafanyakazi wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa
mikataba yao ya kazi na kwa njia hiyo, watakuwa wamejijengea mazingira
mazuri ya kudai haki zao kwa mwajiri.
Aidha,katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Singida,
Saidi Alli Amanzi, Dk.Kone alisema ombi la wafanyakazi la kupunguziwa
kodi kutoka kwenye mishahara yao,amelichukua na atalifikisha kwenye
mamlaka zinazohusika.
“Kwa
ujumla, nimeyapokea mengi mliyowasilisha kupitia risala yenu. Yapo
ambayo serikali ya mkoa itahitaji kufanya mawasliano na mamlaka
mbalimbali husika au wizara, ili kutatua kero hizo, kikubwa muwe na
subira na wakati huo huo, endeleeni kuchapa kazi kwa bidii wakati kero
zenu zinatafutiwa ufumbuzi”,alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Katika
hatua nyingine, Dk.Kone alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji
waliokabidhiwa dhamana ya kuhudumia watumishi,kuacha mara moja matumizi
ya lugha ambazo hadhirizishi mbele ya watumishi wa chini yao, kwa vile
lugha chafu pia inakatisha tamaa watumishi wa ngazi za chini.
“Aidha,
katika risala yenu imeelezwa kwamba kuna baadhi ya halmashauri hazina
mabaraza ya wafanyakazi kabisa,hii ni kukiuka agizo la Rais na
hazijaunda mabaraza ya wafanyakazi, kufanya hivyo haraka
iwezekanavyo,ili kuwapo fursa wafanyakazi wao kupata sehemu ya kusemea
matatizo yao”,alifafanua Dk.Kone.
Awali
mratibu wa shehere hizo ambaye ni katibu TUICO mkoa wa Singida, Edwin
Nampesya,alisema TUCTA inasikitishwa na uongozi wa hospitali ya
Kilimantinde inayomilikiwa na kanisa Anglican, hospitali ya misheni ya
kijiji cha Puma na ile hospitali ya Lutheran ya Iambi, kukataa kutambua
vyama vya wafanyakazi, kitendo kinachosababisha wafanyakazi wakose
mahali pa kusema matatizo yao.
“Cha
kusikitisha zaidi ni pale wafanyakazi wanapotaka kuunda tawi
lao,huonekana kama maadui wakubwa na kutishiwa kufukuzwa kazi. Tunaomba
uongozi wa serikali mkoa uingilie kati suala hili kwa umakini”,alisema
Nampesya.
Kupitia
risala yao wafanyakazi wa mkoa wa Singida,wameomba zoezi la kupiga kura
lifanyike siku ya Jumatatu, Jumanne, Jumatano,Aalhamisi na lisiguse
kabisa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili,ili kutoa nafasi kwa waumini
kufanya ibada bila bugudha yoyote
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269