Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ( Mb), akizungumzia namna Tanzania inavyotekeleza Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4All) wakati wa Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Sekta ya Nishani, uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, jana, Alhamisi.
Na MwandishiMaalum, New York
Tanzania inaamini kwamba,
utekelezaji wa mipango na malengo mbalimbali ya maendeleo hayataweza kupatika au kufikiwa kwa haraka pasipo na uwepo wa nishati endelevu kwa wote.
Ni
kutokana na kulitambua hilo, Tanzania
imejikita kikamilifu katika kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja na kuongeza maradufu kiwango
cha uboreshaji na ufanisi wa nishati mbadala ili kuchagiza maendeleo.
Hayo yameelezwa siku jana Alhamisi, na Naibu Waziri wa Nishatina Madini, Mhe. Charles
Kitwanga ( Mb), wakati wakizungumza katika siku ya pili
ya majadiliano ya mawaziri wanaohusika na sekta ya nishati ambapo kila waziri aliyehudhuria mkutanohuo alipata fursa ya kuelezea na kutoa ahadi ya namna inavyotekeleza mkakati wa nishati endelevu wa wote
(SE4All).
Mhe. Kitwanga naujumbe
wake unaowashirikisha wataalamum balimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini akiwamo Kaimu Katibu Mkuu,
Bw. Ngosi Mwihava wameshiriki kikamilifuka katika mkutano huu ulioitishwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon, ambapo tangu ulipoanza mapema wiki hii,
washiriki wamekuwa wakijadili mada mbalimbali zinazohusiana na masuala ya nishati, uwekezaji na mchango wake katika eneo zima la
utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.
“ Tanzania inaamini kwamba hakuna ajenda za maendeleo zinazoweza kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wanishati ya uhakika”
akasemaNaibu Waziri
Nakuongeza kuwa, mkakati wa nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali inayohitajika ili kufika malengo ya kitaifa ya nishati endelevu kwa wote kufikia mwaka
2034 kama inavyoainishwa katika mkakati huo.
Kwa mujibu wa Naibu
Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania
ilipitisha mkakati wa SE4All mwaka 2012 na kufuatiwa na mchakato wa kufanya tathmini ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea
kutoa taarifa ya tathmini mwaka 2013
Baada ya tathmini hiyo ilifuatia misaada kutoka
SE4All kwaajili ya Afrika iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na nchi ( Country Action Agenda) kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo
ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP).
Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga, taarifa
hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa
udhibitisho mwezi Agosti, 2015.
Aidha maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji umeanza na utalenga katika kuangalia
mahitaji ya haraka ili kuwezesha mpango huo kuanza kutekelezwa.
Kitwanga akiteta jambo na Mwakilishi wa Bank ya Maendeleo kwaajili ya Afrika AfDB muda mfupi mara baada ya Naibu Waziri kuzungumza , mkutano huu wa SE4All, pamoja na Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa vyombo vya fedha kama vile Bank ya Dunia, AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika nishati endelevu.
.Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava akiwasilisha Action Agenda of Tanzania kuhusu SE4All katika moja ya mikutano iliyofanyika hapa jijini New York.
Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava akiwa na wataalamu wake na wataalamu washauri wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269