Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akiwasili
kwenye uwanja wa ndege Kigoma akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole (wa pili kulia) na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma
ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru
(wa pili kushoto) kwa ajili ya kutembelea na kuona changamoto katika
maeneo maalum wanapohifadhiwa Wakimbizi. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara
ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala.(Picha
zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Kigoma
Waziri
wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Tanzania itatoa nafasi
zaidi kuliko ya sasa ili kuweza kuwaweka wakimbizi wa Burundi wanaoingia
nchini katika mazingira ya kuishi maisha ya kawaida.
Kauli
hiyo ameitoa ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma jana kabla ya kuelekea
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kujionea hali ilivyo akiambatana na
watendaji wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini.
Alisema
kama taifa wameona uwingi wa Wakimbizi na watatoa nafasi zaidi ili
kuwezesha Wakimbizi hao kupata mahitaji yao ya msingi kwa mujibu wa
taratibu za Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi.
Alisema
katika kufanikisha suala la kuhudumia Wakimbizi wanaomiminika kwa sasa
serikali itashirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha
mahitaji ya msingi kwa Wakimnbizi hao yanapatikana.
“Wakimbizi wanahaki ya kulindwa na kuthaminiwa kama wananchi wa
Tanzania, kwa hiyo serikali itatoa nafasi zaidi na tunashukuru msaada
tunaopata kutoka kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kukabiliana na tatizo
hili …,” alisema.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema kwamba Umoja wa
Mataifa unatiwa shaka na hali ya kisiasa ilivyo nchini Burundi na kusema
kuyumba kwa hali ya kisiasa kunaweza kuleta Wakimbizi wengi nchini.
Alisema
kwa sasa Umoja wa Mataifa unafanya kazi na Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Umoja wa Afrika na wanachama wengine wa jumuiya za kimataifa
kuhakikisha kwamba hali ya usalama inarejea nchini Burundi.
Aidha aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatuliwa kwa mgogoro wa Burundi.
Rodriguez
alisema Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa namna inavyoshughulikia
Wakimbizi na kusema Umoja wa Mataifa unaangalia hali inayojitokeza
Burundi kwa makini ili kusaidia Tanzania isilemewe na Wakimbizi.
Aidha
alisema kwamba kitendo cha serikali ya Tanzania kutoa nafasi zaidi ya
kuwezesha kusiwepo na msongamano wa Wakimbizi Nyarugusu kunaonesha
ushirika wa kweli kati ya serikali ya Tanzania na jumuiya ya Kimataifa
katika kushughulikia matatizo ya Wakimbizi.
Alisema
hata hivyo kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya ni gharama kubwa na kuitaka
jumuiya ya kimataifa kusaidia kuanzishwa kwa kambi hiyo mpya.
Aidha
alisema kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanyakazi kama shirika
moja, chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia
Wakimbizi duniani (UNHCR) wameitikia wanavyostahili pamoja na changamoto
nyingi walizokumbana nazo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akisamiana na Waziri wa
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand
Mtui (kulia) pamoja na viongozi wengine wa usalama wa mkoa wa Kigoma
mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Kigoma akiwa
na mwenyeji wake Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu
Tawala wa mkoa huo, Mhandisi Dkt. John Ndunguru (wa pili kushoto).
Changamnoto
hizo ni pamoja na uwingi wa Wakimbizi waliokuwa wakimiminika, umbali
uliopo wa kambi ya Kagunga ambako walikuwa wanafikia huku waliowengi
wakiwa wanawake na watoto.
Alisema
hata hivyo UNHCR walifanikiwa kuwasajili Wakimbizi hao na kuandaa
mazingira ya ukazi wao katika kambi ya Nyarugusu. Aidha wamewezesha
usafiri kwa Wakimbizi kutoka Kagunga hadi Kigoma.
Pia
alisema IOM walifungua njia kutoka Kagunga hadi eneo jirani ambako
Wakimbizi walipakia katika mabasi na kufika katika vituo walivyotakiwa
kuwepo.
Pia
UNICEF waliweza kusaidia maji na vifaa vya usafi kwa watoto na WFP wao
walihakikisha chakula kinafikishwa hasa biskuti za kuongeza nguvu.
Aidha WHO wao walikuwa wanaisaidia serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Kipindupindu.
Aidha UNFPA walishughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Mratibu
huyo alisema kwamba hata hivyo mambo yote hayo yasingefanikiwa kama si
kwa msaada wa serikali ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Mratibu
huyo alisema kuwa Mashriika ya Umoja wa Mataifa yameanza kupata fedha
za kusaidia katika shughuli zao na kwamba kuna ahadi ya dola za Marekani
milioni 12.
Alisema
kwamba Umoja wa Mataifa umeona kwamba kutitirika kwa Wakimbizi hao
kumeleta hali ngumu kwa serikali ya Tanzania na wakazi wa Kigoma.
Alisema
wanatambua changamoto zinazoambatana na kuwa na kundi kubwa la
Wakimbizi lakini wataendelea kuhitaji msaada wa serikali ya Tanzania na
jumuiya ya kimataifa katika kipindi hiki kigumu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiendelea kusamiana na
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma waliofika kumlaki katika uwanja wa
ndege wa mjini Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la
Polisi mkoani Kigoma Kamishina mwandamizi, Ferdinand Mtui mara tu baada
ya kuwasili akiwa amefuatana na Waziri Chikawe (hayupo pichani).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (kulia) akifurahi jambo
na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner kwenye uwanja wa ndege
mjini Kigoma mara tu baada ya kuwasili.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa
Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux (kulia)
mara tu baada ya kuwasili mjini Kigoma tayari kuelekea kambi ya
Wakimbizi Nyarugusu.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole akifafanua jambo kwa viongozi wenzake mara tu baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kigoma. Wa pili kushoto ni Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Idara ya huduma za
Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (wa pili
kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw.
Damien Thuriaux.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) akiongozana na Mkuu wa
Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Bw. Damien Thuriaux kuelekea
chumba maalum cha mapumziko mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege mjini Kigoma.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akisaini kitabu cha wageni
kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika uwanja wa ndege wa
mjini Kigoma. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias
Chikawe akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la
Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (katikati) walipokuwa
kwenye chumba cha mapumziko.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez wakisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa
mkoa wa Kigoma kabla ya kusomewa kwa taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi
mkoani Kigoma.
Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Katibu Tawala wa mkoa huo,
Mhandisi Dkt. John Ndunguru akisoma taarifa fupi ya hali ya Wakimbizi
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe aliyeambatana
na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa mjini
Kigoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza kwenye
mkutano wa kupokea taarifa fupi ya hali ya wakimbizi katika mji wa
Kigoma na changamoto wanazokabiliana nazo mbele ya wawakilishi wa
Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia jitihada zilizofanywa na
Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
na mashirika mengi katika kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana
kwa haraka zaidi ili wakimbizi nao wafarijike kama binadamu wengine
sambamba na sheria za Umoja wa Mataifa zinavyotaka. Kushoto ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe na watatu kulia ni
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR),
Joyce Mends-Cole.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na mazungumzo na viongozi
mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Kigoma.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole akizungumza katika mkutano huo ambapo ameipongeza serikali ya
Tanzania kwa moyo wake wa upendo na kutenga maeneo maalum ya kuhifadhi
Wakimbizi kutoka nchi za jirani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katika picha ya pamoja
ya viongozi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa mkoa wa Kigoma
sambamba wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa
yaliyopiga kambi mkoani Kigoma kuhudumia Wakimbizi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269