Mlezi
wa chama cha wafanyakazi madereva Tanzania (TADWU), Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na madereva kabla ya
kukabidhiwa rasimu ya maboresho ya maslahi ya madereva hao na cheti cha
utambulisho wa chama hicho Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah Lubara na Mwenyekiti wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Abdallah
Lubara (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda,
rasimu ya mkataba wa maslahi ya madereva waliyokuwa wakiidai serikali
kwa muda mrefu Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa zamani wa Umoja wa Madereva Tanzania, Clement Masanja (kushoto),
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda cheti cha
utambulisho wa chama chao kipya kitakachoitwa Chama cha Wafanyakazi
Madereva Tanzania (TADWU) baada kuundwa rasmi ambacho kitazindulia Julai
Mosi mwaka huu.
Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Rashid Said (kulia) akizungumzia yaliyomo kwenye rasimu hiyo na maboresho ya maslahi yao.
DC Makonda akisalimiana na madereva baada ya kumaliza kwa mkutano huo.
Madereva wakiwa wamesimama wakisubiri kusalimiana na mlezi wao DC Paul Makonda.
Ni usikivu kwa mlezi wao wakati akihutubia.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa madereva hao.
Madereva wakiwa kwenye mkutano huo.
Madereva wakishangilia hutuba ya mlezi wao Paul Makonda.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha Madereva nchini nchini kimemkabidhi mlezi wao Mkuu wa Wlaya ya
Kinondoni Paul Makonda rasimu ya mkataba uliobeba maboresha ya maslahi
waliokuwa wanaidai kutoka kwa wamiliki pamoja na Serikali.
Katika
hatua nyingine madereva hao Julai Mosi mwaka huu wanatarajiwa kuzindua
chama chao ambacho kitaitwa Chama cha Madereva Wafanyakazi Tanzania
(TADWU).
Hatua
ya kutengeneza rasmu hiyo hiyo imekuja baada ya kikao walichokaa Juni
21 mwaka huu ambapo lengo lilikuwa ni kuwashinikiza waajiri kuwapa
mikataba ya kudumu wakiwa kazini ikiwa ni pamoja na likizo za uzazi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu katibu mkuu wa chama
hicho, Rashid Said alisema rasimu ya mkataba huo imebeba maboresho ya
maslahi yao waliyokuwa wanadai.
Alisema
madai hayo ni pamoja na bima ya maisha , mazishi yenye staha, muda wa
kazi kisheria, matibabu, na nauli ya kwenda kazini.
"Leo
tuna chama cha wafanyakazi madereva Tanzania , pia tumepewa mkataba
hivyo nawatangazia madereva wote kuwa tumepata chombo cha kuzungumzia
tofauti na ilivyokuwa awali.
Kwa
sasa imebaki kujadili na serikali kuhusu kuboreshwa kwa mishahara hivyo
napenda kuwatangazia madereva kuwa tumepata mikataba tuliyohitaji miaka
mingi,"alisema.
Katibu
huyo aliongeza kuwa chama hicho hakitasita kumchulia hatua za kisheria
mmiliki atakayekiuka sheria hizo na kuongeza hakitasitakumpeleka kwenye
vyombo vya sheria kama walivyokuwa wanawafanyia mwanzoni.
Akikabidhiwa
mkataba huo kwa chama hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
alisema mahali walipofikia madereva hao kwa sasa ni jambo la kuleta
maendele makubwa.
Alisema
watanzania wanatakiwa kutambua kuwa madai hayo si kwa ajili ya madereva
peke yao bali ni kwa ajili ya taifa zima na kwamba kutatuliwa kwa
changamoto hiyo kutapunguza ajali zinazoendelea kutokea nchini.
Makonda
alisema asilimia kubwa ya madereva wamekuwa wakipata ajali kutokana na
kuchoka hivyo wanaposinzia usahau kuwa wanaendesha vyombo vya moto hivyo
kusababisha ajali.
Katika
hatua nyingine Makonda alisema kuwa asilimia 80 ya waandishi wa habari
hawana mikataba ya kudumu na kwamba ni changamoto hivyo aliwataka kwenda
kuonana nae ili kupata ushauri wa namna ya kuwawezesha kuhakikisha
wanapewa mikataba ya ajira na waajiri wao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269