Waombolezaji
wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya
Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club
Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia
juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani
Kagera.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald
Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson
Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari
na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya
kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu
Wanahabari ni huzuni na vilio
Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati
wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi
wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo,
Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa
mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa
mikataba ya ajira kwa wanahabari.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald
Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea
alikuwa akifanyakazi marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269