Breaking News

Your Ad Spot

Jun 23, 2015

NEC YATISHIA KUSITISHA ZOEZI LA UANDIKISHAJI ARUSHA NA KILIMANJARO

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini NEC imetishia kusitisha zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika miji ya Arusha na Kilimanjaro endapo viongozi wa kisiasa wataendelea kuingilia mchakato huo na kuwa vyanzo vya vurugu katika vituo vya kuandikishia.
Ni mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Damiani Lubuva akielezea masikitiko ya tume kufuatilia kile alichokiita ni kuingiliwa kwa maafisa wa tume katika kazi zao za uandikishaji katika miji ya Arusha na Kilimanjaro jambao lililopelekea kuzuka kwa vurugu katika baadhi ya vituo ndani ya mikoa hiyo.
Jaji Damian amesema katika mahojiano yake maalum na ITV jijini Dar es Salaam, kuwa tangu kaunza kwa zoezi la uandikishaji kumekuwa na changamoto kadha ambazo hata hivyo tume ilijitahidi kuzitatua lakini kwa hali ya Arusha na Kilimanjaro huenda tume ikalazimika kufanya maamuzi magumu.
Amesisitiza kuwa ni vema viongozi wa kisiasa wakahakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kufanikisha zoezi hilo ambalo kwasasa limekwisha kukamilika kwa zaidi ya asilimia 85, ambapo pia amesisitiza kuwa kwa hali ilivyo hivi sasa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa kwani kila kitu kiko katika hali ya ukamilifu.
Katika mahojaino hayo pia jaji Lubuva amezungumzia suala la uandikishwaji kwa upande wa Zanzibar ambapo anasema zoezi hilo linatarajia kuanza muda wowote akuanzia sasa huku akisisitiza utulivu wakati wa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages