Nigeria imeendelea kukumbwa na matukio
ya vifo, baada ya tukio la kundi la Boko Haram kuvamia msikiti na kuuwa
watu 16 jana, kuna taarifa nyingine ambayo si nzuri kutoka nchini humo.
Watu
wasiopungua 70 wamefariki dunia Mashariki mwa Nigeria baada ya lori la
kubeba mafuta kushika moto huku magari mengine 15 nayo yakishika moto.
Mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea jana
wamesema dereva wa gari hilo alishindwa kudhibiti mwendo kazi wa gari
hilo ndipo likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu
waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.
Miaka mitatu iliyopita ajali mbaya kama
hiyo iliua zaidi ya watu 100 huko Niger katika ajali ilisababishwa na
watu kuchota mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata
ajali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269