Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I),
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil,
wakati wa sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa
Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto),
akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil, baada ya kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema
Daraja la (I), katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye
Ukumbi mpya wa Mikutano Ikulu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watatu kushoto) akiwa na baadhi ya
Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri kutunukiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kwenda nyuma mstari wa kwanza)
akiwa na baadhi ya Watunukiwa wakiwa katika hafla hiyo wakati wakisubiri
kutunukiwa. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
(IGP) Ernest Mangu (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya
Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete,
katika sherehe ya kutunuku Nishani iliyofanyika kwenye Ukumbi mpya wa
Mikutano Ikulu,
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
(CGP) John Minja (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani ya Utumishi
Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil baada ya kutunukiwa Nishani
ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I) na Rais Jakaya Kikwete.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akiteta jambo na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR),
Joyce Mends-Cole katika Ukumbi Mpya wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es
Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtunukia Katibu Mkuu huyo,
Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa
Jeshi la Magereza nchini, (CGP) John Minja (kulia) na Mkurugenzi wa Sera
na Mipango, wa Wizara hiyo, Haji Janabi, nje ya Ukumbi mpya wa Mikutano
Ikulu, jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete
kumtunuku Katibu Mkuu huyo, Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema
Daraja la (I).
Rais Jakaya Kikwete (wanne kushoto
mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Watunukiwa wa Nishani
ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la Kwanza. Wakwanza kulia
mstari wa nyuma ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu,
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269